Jeshi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limesema kuwa zaidi ya watu mia tano wameuawa katika mapigano kati ya vikosi vya usalama na vile vinavyoipinga serikali tokea mwishoni mwa mwezi Machi.

Takriban wanajeshi mia nne kati ya waliouawa ni wafuasi wa Kamuina Nsapu , kundi ambalo linashambulia vitu vyote vinavyohusiana na serikali.
Wanaosalia ni wanajeshi wa serikali na polisi.
Zaidi ya watu milioni moja wameyahama makazi yao katika mkoa wa Kasai tokea kuanza kwa mapigano hayo miezi tisa iliyopita.
Zaidi ya makaburi ya pamoja 40 yamekutwa katika eneo hilo.