Manchester United ilinusurika katika dakika za mwisho za mechi yao dhidi ya klabu ya Celta Vigo kutoka Uhispania na kuweza kufuzu kwa fainal ya kombe la Yuropa.
United itacheza dhidi ya Ajax Amsterdam ya Uholanzi ambayo ilifuzu kwa kuishinda Lyon ya Ufaransa.
Ikiwa kifua mbele kwa 1-0 ugenini United ilipata bao lao kupitia Marouane Fellaini aliyefunga kwa kichwa kufuatia krosi ya Marcus Rashford.
Lakini Celta Vigo iliohitaji mabao mawili ili kufuzu ilisawazisha kupitia Facundo Roncaglia na kuifanya nusu fainali hiyo kuwa na tumbo joto.
Mlinzi wa United Eric Baily na Roncaglia walipewa kadi nyekundu baada ya kuzua ghasia uwanjani huku Man United ikilinda ushindi huo na kufuzu fainali.
Hatahivyo walisheherekea baada mshambuliaji wa Celta Vigo John Guidetti kukosa fursa nzuri ya kupata ushindi wa kuwaweka mbele wageni hao katika kipindi cha lala salama.
Jumla hiyo imesaidia Manchester United kufuzu katika fainali na hatua nzuri ya kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya .
Watakutana na Ajax ambao waliwashinda Lyon katika nusu fainali nyengine katika mji wa Stockholm mnamo mwezi Mei 24.
|
0 Comments