Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 14, 2017

Korea Kaskazini yalifanyia jaribio kombora la masafa marefu

Kumekuwa na shutma kubwa kote duniani dhidi ya hatua ya hivi punde ya Korea Kaskazini, kufanyia majaribio yake zana za nuklia
Marekani inataka vikwazo zaidi viongezewe taifa hilo huku Ikulu ya White House ikisema kuwa, Pyongyang imechwa kutekeleza upumbavu kwa muda mrefu.

Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in, amelaani kitendo hicho cha Korea Kaskazini, cha kufanya majaribio zaidi ya zana zake za mafasa marefu, akilitaja kama kitendo cha uchochezi.
Jeshi la Marekani limetihibtisha kuwa kombora hilo la masafa marefu, lilirushwa karibu na mji wa kaskazini magharibi wa Kusong na kuanguka katika bahari ya Japan.
Kombora hilo lilianguka katika bahari ya Japan
Image captionKombora hilo lilianguka katika bahari ya Japan
Moon ambaye alisema anataka ushirikiano zaidi na utawala wa Pyongyang, wakati wa kampeni yake, amejibu hatua hiyo kwa kuitisha mkutano wa dharura na washauri wake wa kiusalama.
Jaribio lingine la Korea Kaskazini la kuifanyia majaribio zana hizo, liligonga mwamba wiki mbili zilizopita.
Korea Kaskazini imekiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa pamoja na vikwazo na kufanya majaribio matano ya zana zake za masafa marefu za nuklia.
Jaribio hilo linakuja siku chache baada ya rais mpya kushika usukani Korea KusiniHaki miliki ya pichaEPA
Image captionJaribio hilo linakuja siku chache baada ya rais mpya kushika usukani Korea Kusini


Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP