Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg
John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo ulioongozwa
na Mchungaji kiongozi wa usharika huo, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya
Pwani, Kiongozi wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo na baadhi ya wazee wa kanisa.
Leo tarehe 23, Mei 2017





Muonekano wa ukuta wa kanisa la KKKT Usharika wa Ubungolinalotakiwa kuvunjwa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg
John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini maelezo ya viongozi wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo wakati wa kikao cha pamoja cha maridhiano ya utatuzi wa mgogoro wa Eneo la ardhi. Leo tarehe 23, Mei 2017




Darasa lililokabidhiwa na Uongozi wa kanisa la kiinjili la Kilutheli Tanzania Usharika wa Ubungo kwa Uongozi wa Manispaa ya ubungo mbele ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg john Lipesi Kayombo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg
John Lipesi Kayombo akikagua majengo ambayo yamejengwa na kanisa la KKKT yakiwa yameingia katika eneo la shule ya Msingi Ubungo Plaza sambamba na viongozi wa kanisa hilo baada ya kikao cha pamoja na Uongozi wa
Kanisa hilo Usharika wa Ubungo.
Leo tarehe 23, Mei 2017



Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg
John Lipesi Kayombo akisalimiana na Mchungaji kiongozi wa kanisa La Kiinjili la Kilutheli Tanzania Mchungaji Goodlisten Nkya alipozuru katika ofisi za kanisa hilo kwa ajili ya kikao na Uongozi wa  (KKKT) Usharika wa Ubungo.
Leo tarehe 23, Mei 2017



Muonekano wa Majengo ya Shule ya Msingi Ubungo Plaza yatakayofanyiwa marekebisho mara baada ya ujenzi wa Madarasa nane kukamilika

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg
John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo ulioongozwa
na Mchungaji kiongozi wa usharika huo, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya
Pwani, Kiongozi wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo na baadhi ya wazee wa kanisa.
Leo tarehe 23, Mei 2017



Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg
John Lipesi Kayombo akizungumza akizungumza na Afisa Mtendaji wa Kata ya Ubungo,Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa National Housing, Waalimu wa Shule ya msingi ubungo Plaza sambamba na viongozi wengine mara baada ya kikao na Uongozi wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo.
Leo tarehe 23, Mei 2017



Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg
John Lipesi Kayombo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzuru kwa katika ofisi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo leo
tarehe 23, Mei 2017



Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ubungo Ndg
John Lipesi Kayombo akikagua majengo ambayo yamejengwa na kanisa la KKKT
yakiwa yameingia katika eneo la shule ya Msingi Ubungo Plaza sambamba
na viongozi wa kanisa hilo baada ya kikao cha pamoja na Uongozi wa
Kanisa hilo Usharika wa Ubungo.
Leo tarehe 23, Mei 2017.




Na Mathias Canal, Dar essalaam










Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg
John Lipesi Kayombo Leo tarehe 23, Mei 2017 amefanya mazungumzo na Uongozi wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo ulioongozwa
na Mchungaji kiongozi wa usharika huo, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya
Pwani, Kiongozi wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo na baadhi ya wazee wa kanisa.







Kikao hicho kilichofanyika katika
ofisi za usharika wa KKKT Ubungo kilikuwa na Agenda ya kujadili nanma bora ya
uvunjaji wa Ukuta wa eneo la kanisa hilo ambao umeingia katika eneo la Shule ya
Msingi Ubungo Plaza Jambo linalopelekea Kushindwa kuanza ujenzi wa madarasa
nane mapya kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo ambao kwa sasa wanasoma katika
madarasa ambayo majengo yake si rafiki kwa ajili ya usomaji.




Alisisitiza kuwa ujenzi huo utakuwa
maalumu kwa ajili ya kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare
Makori alilolitoa
Mei 19, 2017 wakati wa
mkutano wake na walimu wa shule hiyo sambamba na wananchi wa Mtaa huo
ukiwajumuisha

Afisa mtendaji wa Kata na wajumbe wa mitaa.



MD Kayombo alisema kuwa baadhi ya
shule katika Manispaa ya Ubungo hazifanyi vizuri katika matokeo ya mitihani ya
taifa kutokana na uduni wa miundombinu ikiwemo madarasa Jambo ambalo pia
limepelekea Manispaa ya Ubungo kuona umuhimu wa kuboresha miundombinu ili kuwa
rafiki kwa wanafunzi kujifunzia.

Alisema kuwa jukumu la viongozi
wanaomuwakilisha Rais Magufuli katika ngazi za Mitaa, Kata, Tarafa, Wilaya, Mikoa
na Taifa ni kusimamia na kutekeleza matakwa ya jamii kwa kuzingatia sheria na
taratibu za nchi bila kumuonea mtu yeyote.

Aidha ameupongeza uongozi wa kanisa
hilo kwa ushirikiano waliouonyesha na kukubali kuwa na maridhiano ya pamoja
kuhusiana na namna bora ya kutatua mgogoro huo ambapo pia amewaupongeza Uongozi
wa KKKT Usharika wa Mabibo kwa kuamua kutoa moja ya jengo lao kwa ajili ya
shule hiyo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha miundombinu ya
shule ili kukuza ufanisi wa elimu nchini.

Kwa upande wake mchungaji Kiongozi
wa Kanisa la Kiiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo Mch
Goodlisten Nkya amesifu uongozi wa Mkurugenzi Kayombo kwa kukubali kufanya
maridhiano sambamba na kukubali kupokea jengo mojawapo la kanisa hilo walilotoa
sadaka ambalo litatumiwa na shule ya Msingi Ubungo Plaza kama ofisi ya walimu
ama darasa kwa kadri itakavyoamuliwa na uongozi wa shule.

Alisema kuwa adhma ya kanisa hilo ni
kuona maendeleo endelevu ya elimu nchini Tanzania kwa manufaa ya watanzania
wote sambamba na kupongeza ushirikiano wanaoupata kutoka serikalini na katika
Uongozi wa Shule hiyo.