Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Kibamba Chama-Dar es salaam



Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza na Waandishi wa habari

Mwenge
wa Uhuru Mwaka 2017 utawasili kesho Tarehe 31 Mei 2017 katika Wilaya ya Ubungo kuanzia
saa moja kamili asubuhi na kuzuru katika Miradi mitano ya Maendeleo.   
     
Akizungumza
na Waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori
amesema kuwa katika mbio hizo za Mwenge wa Uhuru Mradi mmoja wa kituo cha
Polisi Gogoni utawekwa jiwe la msingi.

Alisema
kuwa Miradi mingine itakayozinduliwa ni Mradi wa Ujenzi wa Jengo la kutolea
huduma za VVU katika Kituo cha afya Mbezi, Uzinduzi wa madarasa nane katika
shule ya Msingi Malambamawili iliyopo Kata ya Msigani, Uzinduzi wa Kituo cha
mabasi SIMU 2000 Kata ya Sinza na Uzinduzi wa Zahaanti ya Mburahati.

Mhe Makori alisema kuwa Miradi yote hiyo
itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 itagharibu Bilioni
2,854,647,991.89



Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori
amewasihi wakazi wa Manispaa ya Ubungo kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa
Uhuru ambao utawasili katika eneo la SAISAI Kata ya Gobaukitokea Manispaa ya Kinondoni.




Pia amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika
Viwanja vya Barafu, Shule ya Msingi Mburahati kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru.




Imetolewa Na:

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo