Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 14, 2017

Rais mpya wa Ufaransa Emmanuel Macron aapishwa

Rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron, anaapishwa hivi sasa, juma moja baada ya kupata ushindi mkubwa katika marudio ya uchaguzi mkuu wa Urais nchini humo.

Alimshinda pakubwa kiongozi wa chama cha kulia Bi Marine Le Pen.
Bwana Macron, ambaye aliendesha siasa zake akiunga mkono umoja wa Jumuia ya mataifa ya Bara Ulaya, ameahidi kufufua uchumi wa Ufaransa na kufanyia mabadiliko siasa za kale za Ufaransa.
Ili kuafikia mabadiliko zaidi, chama chake kipya cha The Republic on the Move, kinafaa kushinda viti vingi vya ubunge katika uchaguzi wa mwezi ujao.
Mwaandishi wa BBC anasema kuwa, iwapo Bwana Macron, atashindwa katika wadhifa huu wake mpya kama Rais wa Ufaransa, atakuwa tu sawa na mtangulizi wake wa chama cha Kisosiolosti Francois Hollande, ambaye aliahidi mabadiliko, lakini anaondoka kama Rais asiye na umaarufu katika hostoria ya Ufaransa.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP