Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi (Kulia) katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi  iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi Theresia Mmbando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo wakifatilia dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Happi wakijadili jambo katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kushoto), na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Kulia) wakifatilia dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akizungumza jambo na Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Simon Sirro katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi  iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mhariri wa Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Ndg Mathias Canal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Muonekano wa Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam ukitokea Mkoani Lindi.
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda Leo Me 27, 2017
amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi
katika dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika eneo la Kongowe Shule
ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma na kuukabidhi kwa Mkuu wa
Wilaya ya Temeke tayari kwa kumulika miradi ya Maendeleo.

Mara
baada ya kukagua Miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Temeke Mwenge wa
Uhuru utazuru katika Wilaya ya Kigamboni Tarehe 28/05/2017, Siku ya
Tarehe 29/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Ilala, Tarehe 30/05/2017
utakimbizwa katika Wilaya ya Kinondoni na Tarehe 31/05/2017 utakimbizwa
katika Wilaya ya Ubungo.

Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mhe Paul C. Makonda amesema kuwa Mwenge wa uhuru ni chombo
kilichoasisiwa na baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka
1961 ikiwa ni Tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika
hivyo kuzuru katika Mkoa wa Dar es salaam itakuwa ni kichocheo kikubwa
katika kuhamasisha Maendeleo, Uzalendo, Umoja , Mshikamano na kudumisha
Amani ndani na nje ya Taifa letu.

Mhe
Makonda alisema kuwa Mwaka huu utakuwa mwaka wa 24 tangu mbio za Mwenge
wa Uhuru zirejeshwe chini ya utaratibu wa usimamizi wa serikali kutokana
na mabadiliko ya kidemokrasia baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa
vyama vingi vya siasa mwaka 1992.

Katika
mapambano dhidi ya Dawa za kulevya Mhe Makonda alisema kuwa jitihada ya
kudhibiti kusambazwa na Matumizi ya Dawa za Kulevya ni kuifanya kuwa
ajenda muhimu kiutekelezeji kwa mustakabali wa maisha ya watanzania kwa
kuwa Jambo hilo linagusa nguvu kazi ya Taifa.

Rc
Makonda amebainisha kuwa jumla ya Miradi 40 itapitiwa na Mwenge wa
Uhuru kwa Mwaka 2017 katika Mkoa wa Dar es salaam ikiwa na  thamani ya
Shilingi Bilioni 244,392,530,334 ambapo Miradi 12 itazinduliwa, Miradi
15 itawekewa mawe ya Msingi, Miradi miwili itafunguliwa na Miradi 11
itatembelewa.

Mhe Makonda amewapongeza
wananchi wa Mkoa wa  Dar es salaam kwa kujitokeza kwa wingi kuulaki
Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili huku akitoa wito kwa Wakazi wa
Manispaa ya Temeke, Kigamboni, Ilala, Kinondoni na Ubungo kujitokeza kwa
wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru katika maeneo yote utakapozuru kwani
pamoja na mambo yote Mwenge wa Uhuru ni urithi na nembo ya umoja katika
maendeleo yetu.

Awali akizungumza
kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey
Zambi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John
Pombe Magufuli kwa weledi wake katika utendaji hususani katika kudumisha
amani na kuchagiza ukuzaji wa uchumi wa nchi kwa kutilia msisitizo
uwajibikaji serikalini, Kukemea wizi na Ubadhilifu wa Mali za umma
sambamba na Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya.

Mhe
Zambi alisema kuwa Wananchi wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli
katika mapambano dhidi ya wizi wa Mali za Watanzania hususani Vita  ya
kiuchumi aliyoianza hivi karibuni kwa kuzuia Mchanga wa dhahabu
kusafirishwa kwenda nje ya nchi. 

Mhe
Zambi ametoa pongezi hizo kutokana na maamuzi yaliyofanywa na Rais
Magufuli mara baada ya kupokea Ripoti ya kamati iliyokuwa inachunguza
Hatma ya mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Magufuli Machi 29 mwaka
huu ikiwajumuisha Profesa Abdulkarim Hamisi Mruma (Mwenyekiti), Profesa
Justiania Rwezaura Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dokta Yusuph
Ngenya, Dokta Joseph Yoweza Phili, Dokta Ambrose Itika, Mohamed Zengo
Makongoro na Hery Issa Gombela.

Mwenge
wa Uhuru utamaliza mbio zake mkoani Dar es salaam siku ya tarehe
31/05/2017 na kukabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Pwani siku ya tarehe
01/06/2017 katika Uwanja wa kimataifa wa  Mwalimu Julius Nyerere
Terminal 1 kwa ajili ya kuelekea Mafia Mkoani Pwani.

MWISHO