Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 27, 2017

Nakutakieni Mfungo mwema Waislamu wote Duniani

Mwezi wa 9 katika kalenda ya kiislamu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao ni maarufu zaidi kutokana na ibada ya Saumu.
Katika mwezi huu waislamu hutakiwa kufunga kutoka Machweo mpaka Machwa (Mawio) katika kipindi ambacho hawatakiwa kula wala kunywa chochote.

Mwezi wa Ramadhani ni muhimu kwa waumini was dini ya kiislamu kwa kuwa ndio mwezi ulioteremshwa Kurani na pia hufahamika kama mwezi wa Kurani.
Mbali na kujiepusha na kunywa na kula Muislamu hutakiwa kujiepusha na maovu na matendo ya dhambi na kuongeza katika matendo ya ibada kama Swala, Kusoma Kurani, kutoa sadaka na kadhalika.
Katika nchi nyingi duniani mwezi huu unaanza hivi leo tarehe 27 mwezi Mei mwaka wa 2017.
Ramadan Mubaraq
Mathias Canal
0756413465
Dar es salaam
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP