Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 3, 2017

Serengeti Boys yabadilishiwa kituo-Fainali za Afrika kwa vijana

Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys, imebadilishiwa kituo kutoka Port Gentil na sasa imepangiwa mjini Libreville Gabon wakati wa fainali za Afrika kwa vijana.

Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Niger, Angola na Mali ambako watafungua la michuano hiyo Mei 15, mwaka huu, Kwa mabadiliko hayo, Kundi A lenye timu za Cameroon, Ghana, Guinea pamoja na wenyeji Gabon itakuwa mjini Port Gentil.
Kwa sasa Serengeti Boys wako Cameroon kwa kambi ya wiki moja iliyoanza Aprili 29, mwaka huu ambako tayari imecheza na wenyeji Cameroon mchezo mmoja na kushinda bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jijini Yauonde.
Wenyeji hao, Cameroon watarudiana na Serengeti Boys katika mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika leo Jumatano, Mei 3, mwaka huu.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP