Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Real Madrid Christiano Ronaldo amekuwa mwiba mchungu baada ya kuiwezesha timu yake ya Real Madrid kuichapa Atletico Madrid mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliopigwa hapo jana jumanne katika dimba la Estadio Santiago Bernabeu jijini Madrid.

realHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRonaldo alipopachika bao la kwanza katika dakika ya 10 kipindi cha kwanza
Ronaldo alipachika mabao hayo katika dakika ya 10 kipindi cha kwanza na kuandika bao la pili dakika ya 73 kipindi cha pili ,huku akihitimisha karamu ya mabao matatu dakika ya 86 kipindi cha pili.
MadridHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBao la pili katika dakika ya 73
Na hii leo jumatano usiku inatarajiwa kupigwa nusu fainali nyingine kati ya Fc Monaco dhidi ya Juventus huko Stade Louis jijini Monaco.
Na wakati huo huo Mshambuliaji nyota wa Fc Monaco Radamel Falcao amesema hana mpango wowote wa kuondoka katika klabu hiyo ambayo inafukuzia mataji mawili msimu huu, la Ligue 1 na Ligi ya Mabingwa Ulaya.