MSANII Q-Boy Msafi aliyekuwa akifanya kazi kwenye lebo ya WCB, amejikuta akimwaga chozi katikati ya interview na Global TV Online baada kuelezea mazingira halisi ya namna alivyoondoka WCB.
Katika mazungumzo hayo ambapo alikua akizungumzia kazi zake za muziki, pamoja na ku-design mavazi kwa ajili ya kumvalisha Diamond Platinumz, Q-Boy alisema kuondoka kwake WCB siyo kwamba amefukuzwa kama baadhi ya watu wanavyozusha mitandaoni, bali ni mipango yake mwenyewe hivyo anatafuta channel nyingine ambazo zinaweza kumpaisha zaidi.
“Ujue pale WCB kuna wasanii kama watano, yupo Harmonize, Rayvanny, Rich Mavoko, Queen Darleen pamoja na CEO mwenyewe ambaye ni Diamond. Kwa hiyo na mimi nikiongezeka tunakuwa sita. Ikitokea kila mtu ana-project yake yawezekana kwa mwaka ukajikuta unatoa wimbo mwezi wa 12.”
“Tukio ambalo siwezi kulisahahu ni pale unapomfanyia mtu kazi ukiwa na imani na matumaini kwamba kesho unaweza kufaidi, halafu ikaonekana umetumia nguvu na akili nyingi na ukajikuta hufikii malengo.”(AKAMWAGA MACHOZI).
Kauli yake kwa WCB
“Kila mwanadamu ana malengo ya baadaye, yanayoweza kufanya aishi vizuri na familia yake ya baadaye, kitu kibaya ni pale anapotokea mtu anakutoa kwenye malengo, sasa sijui ilikuwa ni maneno tu ya ahadi zao kwamba nifanye kazi.
“Mimi bado ni kijana, bado nina nguvu, nitapigana ili nifikie malengo yangu, lakini wasisahau kama mimi pia ni binadamu, naweza kukosea pia…,”alisema Q-Boy.
0 Comments