Na Elvan Stambuli
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamadi jana ametoa salam za rambirambi kutokana na vifo vya wanafunzi 29 , walimu 2 na dereva mmoja vilivyotokea Arusha.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi pamoja na Global TV, Maalim Seif alisema amesikitishwa na vifo hivyo na amewataka wafiwa wote kuwa na moyo wa subira na akawaombea kwa Mungu waliopoteza maisha.
“Ni wakati ambao inatakiwa serikali iwe wakali kwa madereva wazembe.
Marekani dereva anaogopa kuvunja sheria kutokana na sheria zao kuwa kali, anapigwa faini za kama dola 300. Kila dereva nchini anatakiwa kuzingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali kama hizi,” alisema.
Aliwataka polisi wa usalama barabarani kusimamia sheria ipasavyo ili kuepusha vifo vya ajali kama vilivyotokea Arusha.Na Elvan Stambuli
|
0 Comments