Milolongo mirefu imeshuhudiwa kwenye ofisi za tume ya uchaguzi nchini Kenya, wakati mamia ya watu wakiwemo wabunge na magavana walio ofisini, walifika kujiandikisha kama wagombea huru wakati wa uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti kabla ya siku ya mwisho ya Alhamis.

Wengi wa wale waliofika kujiandikisha ni wanasiasa ambao walishindwa wakati wa uchaguzi wa mchujo na ambao wamevihama vyama vyao kuwa wagombea huru.
Polisi na walinzi walifunga milango ya ofisi za msajili wa vyama ili kudhibi umati uliofika.
"Kuna fujo hapa, tuna karibu maombi 4000 na idadi hiyo inazidi kuongezeka," msajili wa vyama Lucy Ndung'u alisema.
Kati ya wale walio na matumaini ya kuwania ni magava wa sasa wa kaunti za Kirinyaga na Nakuru ambao wote walishindwa wakati wa mchujo wa chama kinachotawala cha Jubilee

Rais Uhuru Kenyatta amewataka wafuasi kuheshimu matokeo ya mchujo.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais Uhuru Kenyatta amewataka wafuasi kuheshimu matokeo ya mchujo.

Wabuge kadha na kati ya wale wanaojiandikisha kuwa wagombea huru baada ya kushindwa kwenye mchujo.
Akizungumzia hatua ya kujiuzulu kwa wanasiasa kutoka chama cha Jubilee, Rais Uhuru Kenyatta aliwataka wafuasi kuheshimu matokeo ya mchujo.
"Mbona watu wananilaumu wakati wapiga kura walifanya uamuzi wao na kuwachagua viongozi wanaowataka? wacha tukubali uamuzi wa wapiga kura," gazeti la Daily Nation lilimnukuu Rais.