Waokoaji nchini Iran wameopoa miili ya watu 21 baada ya kutokea mlipuko mkubwa katika mgodi mmoja wa makaa ya mawe, huku zaidi ya wengine 69 wakijeruhiwa.

Mlipuko huo unadhaniwa kusababishwa na kuvuja kwa gesi katika mgodi wa Zemestan-Yurt Kaskazini mwa jimbo la Golestan.
Waokoaji wakijaribu kupunguza kiwango cha gesi ndani ya mgodi
Image captionWaokoaji wakijaribu kupunguza kiwango cha gesi ndani ya mgodi
Baadhi ya miili hiyo ni ya watu waliokwenda katika mgodi huo kuwasaidia waliojeruhiwa.
Zaidi ya wachimbaji wengine 32 wamekwama ardhini.
Magari ya huduma ya kwanza yakisubiri majeruhi kuwapeleka hospitalini
Image captionMagari ya huduma ya kwanza yakisubiri majeruhi kuwapeleka hospitalini
Juhudi za uokoaji zinaendelea huku zikikwamishwa na njia nyembamba ya kuingia sambamba na uwepo wa kiwango kikubwa cha gesi ndani ya mgodi huo.