Wa kwanza kulia ni mwakilishi wa chama cha
wamiliki wauza mafuta
rejareja  Kanda ya kaskazini  Deipyen Bameda  (TASDOA )
katikati ni
Katibu mkuu  TASDOA Tinno Mmasi akiwa anafafanua jambo mara baada ya
kumkabidhi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Rambirambi zao za vifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent

 Dare salaam
Independent School (DIS) Anna Msangi akiwa anakabidhi kiasi cha
shilingi milioni tatu kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ikiwa ni
mchango wao kwa wanafunzi wa
Lucky
Vicent
mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akifafanua
jambo ofisini kwake kabla ajapokea rambirambi
hizo

Habari picha
na  Woinde Shizza,Arusha



Baadhi ya
 Wanasiasa
wametakiwa kuacha  mara moja kuchulia
tukio la vifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent kama sehemu yao ya
kujinufaisha  kisiasa, pamoja na baadhi yao kupotosha jamii
kupitia  mitandao ya kijamii .





Hayo
yamebainishwa jana  na mkuu wa mkoa wa Arusha  Mrisho Gambo
wakati alipokuwa akipokea rambirambi
za wanafunzi  32 wa Lucky Vicent,zilizotolewa
na chama  cha wamiliki  wauza mafuta rejareja (TASDOA)
pamoja  na uongozi wa shule binafsi ya Dare salaam
Independent School (DIS) ambapo alisema kuwa anasikitishwa sana na baadhi ya
viongozi kuchukulia swala hili kama ni sehemu ya kujijengea
umaarufu.








Alisema kuwa
swala hili sio tukio la kisiasa bali ni mtihani
na changamoto kubwa iliyozikumba familia za wananchi wa Arusha ,hivyo
linatakiwa kuheshimika na kuchukuliwa kama ni tatizo kubwa lililowakumba
wananchi wa mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kwani kuwapoteza watoto hawa
ni jambo  la kusikitisha sana kwani walikuwa
wanategemewa kuwa viongozi wa baadae.





“pia napenda
kuchukuwa fursa hii kuwashukuru kwa kuleta
michango yenu kwa ajili ya wanafunzi hawa 32 ila napenda pia kuwakumbusha
kuwa  jumla ya watu wote waliopata tatizo
walikuwa 38 lakini kati yao waliokufa ni 35 na
na wingine watatu ni majeruhi hivyo napenda kuwasihi wananchi na
mashirika ambayo wanaleta msaada wasiangalie waliopoteza maisha tu bali
wawakumbuke na wale majeruhi watatu ambao wapo nje kwa matibabu kwani wao pia
ni binadamu”alisema Gambo





Alisema kuwa
japo kuwa majeruhi wale waliopelekwa nje
kutibiwa wanaudumiwa bure lakini kuna wale watu ambao wameenda nao pamoja ya
kuwa wanahudumiwa chakula na malazi lakini kwa binadamu waka waida anatakiwa
kujitegemea kwa vitu vidogovidogo hivyo ni vizuri kama watu wanaotoa msaada
wata wakumbuka na hawa majeruhi .





Kwa upande
wake katibu mku u wa  chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja
(TASDOA) Tino Mmasi alisema kuwa wao kama wamiliki wawauza mafuta wadogowadogo
wameguswa sana na msiba huu na ndio maana walioamua kukaa kama wanachama na
kuchanga fedha hizi kiasi cha shilingi millioni saba laki saba
ili ziwafariji wafiwa hawa 35 na pia wameaidi
kwend a kujichanga tena  kwa ajili ya
kuwachangia majeruhi ambao wapo Marekani





“tumetoa hiki
kidogo lakini kwa jinsi  tulivyoguswa tutaenda kuchanga fedha
zingine
kwa ajili ya majeruhi waliopo marekani na tunapenda kukuaidi mkuu wa mkoa
tutakuwa nanyi bega kwa bega hadi majeruhi hawa wote wapone na warudi hapa
nchini”alisema  Mmasi





Katika
michango hii shule ya
shule binafsi ya Dare salaam Independent School (DIS) ilichanga kiasi
cha shilingi  milioni tatu  laki moja na nusu  huku
chama cha wamiliki wa uzamafuta rejareja
wakiwa wamechangia shilingi milioni saba laki saba  huku wote
wakiaidi kwenda kukusanya fedha
nyingine kwa ajili ya majeruhi.