Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa nchini Ufaransa kwa mkondo wa pili muhimu wa uchaguzi wa Urais.
Mwezi uliopita, wapigaji kura waliwakatalia mbali wagombea kiti cha urais wa vyama vikuu viwili, kile cha Kisosiolosti na cha mrembo wa Republican wa kati-kulia.
Leo Jumapili, watamchagua kati ya muungwaji mkubwa wa muungano wa jumuia ya bara Ulaya, Emmanuel Macron na kinara wa mrengo wa kulia Bi Marine Le Pen.
Huku kampeini za uchaguzi mkuu zikimalizika siku ya Ijumaa, Bwana Macron alilengwa na mashambulio ya udukuzi wa kimitandao.
Emmanuel Macron na mpinzani wake wa karibu Bi Marine le Pen, wamezuiwa na sheria za uchaguzi kutoa matamshi ya aina yoyote, kuhusiana na ufujaji wa taarifa hiyo ya mashambulio ya kimitandao.
Lakini, Rais anayeondoka Francois Hollande ameapa kukabiliana vilivyo na wahusika katika udukuzi huo wa kimitandao.
Kamati ya kampeni ya mmoja wa mgombea wa urais nchini Ufaransa, Emmanuel Macron, imesema kuwa imevamiwa vikali na makundi ya udukuzi ambayo yamechapisha habari muhimu ya kundi lao katika mitandao ya kijamii.
Washiriki wa Bwana Macron wamesema kuwa barua pepe sahihi zimeibwa katika tarakilishi zao na kuchanganywa na zile bandia ili kuonyesha kuwa kamati hiyo ya Bwana Macron ni ya ubabaishaji tu.
Chama cha Bwana Macron kijulikanacho nchini kama "En Marche" kilisema kuwa wachapishaji wa habari hizo zilizovurugwa wana nia ya kuvuruga demokrasia kabla ya uchaguzi wa marudio ya hapo kesho.
Tume ya Uchaguzi nchini Ufaransa inatarajiwa kuongoza mkutano wa dharura baadaye hii leo kujadili madai hayo ya udukuzi.
0 Comments