Mmoja wa watu wanaodhania walizaliwa kwa mbegu ya daktari Jan KarbaatHaki miliki ya pichaAFP
Image captionDkt. Jan Karbaat alijiita "muasisi wa fani ya uzazi wa kutunga mimba kwa kupandikiza mbegu ".
Mahakama moja nchini Uholanzi imeidhinisha ombi la familia zinazotaka vipimo vya vinasaba DNA vichukuliwe juu ya mmiliki wa kliniki ya uzazi ya daktari anayeshutumiwa kutumia mbegu zake za kiume katika makumi kadhaa ya kesi.

Jan Karbaat anashukiwa kuwa baba wa watoto wapatao 60 katika kituo cha afya alichomiliki katika eneo la Bijdorp, karibu na Rotterdam.
Vipimo sasa vitafanyika juu ya vifaa vilivyochukuliwa kutoka kwenye nyumba yake baada ya kifo chake mwezi Aprili, akiwa na umri wa miaka 89.
Wakili wa familia yake anasema hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai hayo.
Jan Karbaat alijiita "muasisi wa fani ya uzazi wa kusaidiwa".
Kliniki yake ilifungwa mwaka 2009 wakati kulikuwa na taarifa kwamba alidaiwa kugushi data, uchunguzi na maelezo ya watoaji wa mbegu za kiumena kuzidisha idadi inayoruhusiwa ya idadi ya watoto sita kwa kila anayejitolea kutoa mbegu za uzazi.
Katika kesi ya mahakamani mwezi uliopita, wakili wa wazazi 22 na watoto walisema kwamba visa vinavyoshukiwa vinajumuisha mtoto wa mteja wao mwenye macho ya hudhurungi wakati alikuwa na macho ya blu na mvulana wa mteja wakeambaye anasura inayofanana na daktari.
Taarifa za vinasaba DNA zitasalia kuwa siri hadi pale watoto watakapoonyesha kuwa kuna sababu za kuamini daktari alikuwa baba yao, kulingana na mwandishi wa BBC Anna Holligan, ambaye alikuwa katika mahakama ya wilaya ya Rotterdam.
Hatimae, kama taarifa za vinasaba-DNA zitawiana na watoto hao ambao wengi wao walizaliwa miaka ya 1980s, kutakuwa na tumaini la kumshitaki daktari, labda kwa misingi ya kwamba hawangepaswa kuwepo, ameongeza Anna Holligan.
Joey, ambaye anaamini Jan Karbaat huenda ni baba yake ameiambia BBC: " Ina maana kubwa kwangu ... Tunatumai kupata majibu ."
Wakili wa familia ya Karbaat anapinga kufanyika kwa vipimo vyovyote vya vinasaba DNA.
Wakati wa uhai wake, daktari mwenyewe alikataa kufanya vipimo hivyo.
Hata hivyo, mwezi uliopita,kijana yake Jan Karbaat alitoa vinasaba vyake DNA vipimwe ambavyo vilionyesha kuwa daktari anaweza kuwa babawa watoto 19, waliozaliwa kwa njia ya uzazi wa kutungishwa mbegu kwa lugha ya kitaaamu IVF, kulingana na ripoti ya shirika la habari la AFP.