Wakati ya kipindi cha taaluma yake ya usakataji soka, El Hadji Diouf alipata sifa ya kijana mtukutu wa kandanda.
Sasa akiwa amestaafu, mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal anasema kuwa sifa ya kijana mtukutu wa kandanda haiukuwahi kuwa nzuri.
El Hadji Diouf ni shujaa nchini Senegal na kila mahala anakokwenda hushangiliwa na mashabiki wakiwemo vijana na hata wazee.
Watu nchini Senegal bado wanamshukuru kwa wajibu aliotekeleza wakati wa kombe la dunia mwaka 2002 nchini Japan na Korea Kusini.
Lakini nchini Uingereza anakumbukwa kwa sarakasi zake uwanjani kuliko umahiri aliokuwa nao katika usakataji kandanda.
Ni tabia ililomfuata hadi kwa ligi za Uingereza alipocheza na Liverpool na Blackburn Rovers hadi Bolton Wanderes na Rangers ya Scotland.
Diouf aliwatemea mate wapinzani na kuwakabili wasimamizi wa mechi na wapinzani.
Lakini sasa akiwa amestaafu anaeleza historia.
Mimi ni simba, nina tabia hiyo na ninataka watu waniheshimu.
Diouf ambaye sasa amehamia mji mkuu wa Senegal Dakar, anasema kwa mara kadha hakueleweka vyema wakati wa siku zake akicheza England.
Hata hivyo anakiri amefanya mambo mabaya.
Alipoulizwa na mambo yapi, alisema alikuwa akiwatemea mate wapinzani labda walipomwambia kitu ambacho hakukipenda.
0 Comments