Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 11, 2017

Mazungumzo ya "kigaidi" yasababisha ndege kutua ghafla Ujerumani

Ndege iliyokuwa safarini kutoka Slovania ikielekea Uingereza ilitua kwa ghafla baada ya rubani kujulishwa kuhusu mazungumzo ya kutiliwa shaka yaliyokuwa na matamshi ya kigaidi.

Wanaume watatu raia wa Uingereza waliokamatwa baada ya ndege ya kampuni ya Easyjet kuelekezwa mji wa Cologne, Ujerumani siku ya Jumamosi wanahojiwa.
Abiria wote 151 waliaondelwa na safari za ndege kufutwa kwa muda wa saa tatu.
Mfuko uliokuwa unamilikiwa na wanaume hao ulilipuliwa na polisi.
Msemaji wa uwanja wa ndege wa Cologne alisema kuwa rubani alikuwa amejulishwa kuhusu mazungumzo ya kutiliwa shaka kwenye ambapo aliamua kutua kwa ghafla.
Watu 9 walitibiwa baada ya kushuka kutoka kwa ndege wakitumia milango la dharura ya ndege hiyo Airbus 319.
Kampuni ya Easyjet ilisema kuwa rubani alichukua uamuzi wa kutua kuruhusu ukaguzi wa kiusalama kufanyika.
Watu 9 walitibiwa baada ya kushuka kutoka kwa ndege wakitumia milango la dharura ya ndege hiyo Airbus 319.Haki miliki ya pichaDAVE HARGREAVES
Image captionWatu 9 walitibiwa baada ya kushuka kutoka kwa ndege wakitumia milango la dharura ya ndege hiyo Airbus 319.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP