Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amemkosoa rais wa Marekani Donald Trump akiwa ziarani Mexico.
Amesema kwamba kujenga ukuta sio suluhu la tatizo la uhamiaji.

Matamshi yake yanatokana na ahadi ya Rais Trump ya kujenga ukuta kwenye mpaka kati ya Mexico na Marekani ili kuzuia wahamiaji kutoka Mexico.
Bi merkel pia aliunga mkono msimamo wa Mexico kuhusu biashara huru, kabla ya kuanza majadiliano na Marekani na Canada kuhusu mkataba wa biashara huru na Marekani Kaskazini, maarufu kama NAFTA.
Rais Trump anapinga mkataba huo, na kusema kuwa ataondoka iwapo mkataba huo hautafanyiwa marekebisho yatakayofaidi Marekani.
Hata hivyo rais wa Mexico Enrique Piene Nieto anasema taifa lake litalinda na kuimarisha biashara huru.
Eno la mpaka la Nogales, Arizona katika ya Marekani na MexicoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionEno la mpaka la Nogales, Arizona katika ya Marekani na Mexico