Misri inafunga anga zake kwa ndege za Qatar katika mzozo wa kidiplomasia unaozidi kukua huku Saudi Arabia na Bahrain nazo zikitarajiwa kuchukua hatua kama hiyo leo Jumanne.
Nchi kadha zimekata uhusiano na Qatar, baada ya kuishutumu kwa kuunga mkono ugaidi katika eneo la Ghuba.

Raia wa Qatar nchini Bahrain, Saudi Arabia na Muungano wa Milki ya nchi za kiarabu wamepewa muda wa wiki mbili kuondoka.
Qatar inakana kunga mkono wanamgambo na waziri wake wa mashauri ya nchi za kigeni ametaka kuwepo mazungumzo.
Serikali ya nchi hiyo imesema kwamba mzozo huo hautaathiri chochote katika utaratibu wa maisha , ingawa kuna taarifa za wananchi kuanza kuhifadhi chakula kama dharula tangu mzozo huo ulipoibuka siku ya Jumatatu wiki hii
Nchi ya Saudi Arabia tayari imekwisha tangaza kufungwa kwa mpaka pekee wa aridhini na Qatar
Wakati wa kuchukua hatuahiyo ndege za Saudia na Qatar zitahitaji kuchukua safari ndefu.
Lakini waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Qatar Sheikh Mohammed Bin Abdulrahman al-Thani, alikimbia kituo cha Al Jazeera kuwa ndege zake zinatumia njia za kimataifa za baharini kwa safari za kimataifa.
Afisa mmoja ambaye hakutajwa nchini Somalia aliliambia shirika la AP kuwa takriban ndege 15 za Qatar zimetumia anga ya Somalia siku ya Jumatatu zaidi ya safari za kawaida za kila siku.