Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizikagua jezi alizokabidhiwa na  Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo Plaza Bi Evelyine
Mushi wakati wa dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo uliopo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam




Baadhi ya washiriki wakifatilia kwa karibu dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo uliopo Mtaa wa Kibamba ChamaJijini Dar es salaam



Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa   makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya UMITASHUMTA dhifa iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo uliopo Mtaa wa Kibamba Chama



Meneja Mahusiano Biashara za serikali Bi Mkunde Joseph kutoka Benki ya NMB Makao Makuu akielezea dhamira ya kuchangia vifaa hivyo vya michezo kwa ajili ya wanafunzi wanaoshiriki UMITASHUMTA wakiwakilisha Manispaa ya Ubungo




Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo Plaza Bi Evelyine Mushi akielezea dhamira ya kuchangia vifaa hivyo vya michezo kwa
ajili ya wanafunzi wanaoshiriki UMITASHUMTA wakiwakilisha Manispaa ya
Ubungo,
(Kulia) ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo



Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadau kutoka Benki ya NMB sambamba na watumishi wa Manispaa ya Ubungo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo Plaza Bi Evelyine Mushi wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo Plaza Bi Evelyine Mushi wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo

Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwa kwenye picha ya
pamoja na Wadau kutoka Benki ya NMB sambamba na watumishi wa Manispaa ya
Ubungo




 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo


Na Mathias Canal, Dar es salaam





Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo leo June 2, 2017
amekabidhiwa na Benki ya NMB jezi seti tatu kwa ajili ya wanafunzi wa Manispaa
ya Ubungo.



Jezi hizo zimekabidhiwa kwa Mkurugenzi Kayombo kwa ajili ya maandalizi kwa
wanafunzi wanaotaraji kushiriki katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na
Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA).



Mashindano hayo yanataraji kuanza kurindima June 16, 2017 katika Uwanja wa
CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa kuwakutanisha wanafunzi mbalimbali kutoka kote
nchini Tanzania.



Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa jezi hizo katika dhifa ya makabidhiano
iliyofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Ubungo, Mkurugenzi Kayombo
ameipongeza Bank ya NMB (National Microfinance Bank PLC (NMB) kwa kutoa jezi
hizo kwani Michezo ni moja ya maeneo yanayotumika kutambulisha, kutangaza,
kuipatia sifa nchi na hata utajiri kwa wanamichezo wake.



Alisema kuwa Uendelevu wa michezo huwezekana tu kwa kuenzi mfumo wa kutambua
vipaji kutoka ngazi za chini, kuviibua na kuvikuza hivyo Benki hiyo kuchangia
vifaa hivyo ni dhamira njema katika kuwaunganisha wanafunzi pamoja na kurahisisha
utambuzi wa vipaji vyao.



Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa Njia za makuzi ya watoto zaidi ya nyumbani
na katika jamii zao ni pamoja na elimu rasmi shuleni, ambapo Tanzania kwa miaka
mingi imeweka pia sera ya kutenga muda wa michezo na taaluma nyingine muhimu
kama hii katika shule za msingi.



Alisema Moja ya sifa kuwa za michezo hii, ni kule kushirikisha hata
wanafunzi wenye ulemavu, ambao katika baadhi ya maeneo na timu mitaani wamekuwa
wakikosa nafasi, licha ya kuwa na kipaji na kuwa na uwezo wa kufanya vyema
kuliko wasio na ulemavu.



Kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo Plaza Bi Evelyine
Mushi alisema kuwa UMITASHUMTA kwa miaka mingi imekuwa ikidhaminiwa na serikali
peke yake, na uzoefu umeonyesha wazi kwamba wadau zaidi wanapojitokeza kuchangia
nguvu katika michezo, mafanikio makubwa hupatikana hivyo kuamua kuchangia ni
dhamira njema ya kuunga mkono dhamira ya dhati ya kuanzishwa kwa mashindano
hayo.



Bi Evelyine alisema kuwa wachezaji wanaotamba kwenye michezo mbalimbali
katika ngazi za juu walianzia chini, na laiti vipaji vyao visingetambuliwa na
kukuzwa kwa njia moja au nyingine, ni wazi wsingefikia mafanikio yao.



"Benki ya NMB kuchangia jezi Huko ndiko kuinua michezo, huko ndiko
kulijenga Taifa Tanzania katika jukwaa la kimataifa, na ni tangazo tosha kwa
utajiri wake wa maliasili" Alisema Bi Evelyine



UMITASHUMTA huendeshwa kwa mfumo wa Kanda, ambapo wanafunzi huchujana
kuanzia ngazi za Shule, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa hadi Kanda na kupata timu
ambayo husafiri kuchuana na wenzao katika Mji na Mkoa uliopangwa. Kwa kuwa ni
vigumu kuibua na kukuza vipaji mitaani katika kila kona ya Tanzania,
UMITASHUMTA ni chemchemi bora ya vipaji vya michezo na taaluma, maana ni
mkusanyiko wa waliofanya vizuri tangu ngazi ya chini hadi Kanda