Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. Leo Alhamisi June 1, 2017

Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akitoa taarifa ya Miradi
iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wake mbele ya 
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. Leo Alhamisi June 1, 2017
Baadhi ya Wananchi waliozuru katika dhifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. Leo Alhamisi June 1, 2017
Viongozi mbalimbali wa serikali na wadau akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakifatilia dhifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. Leo Alhamisi June 1, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kwenye dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. Leo Alhamisi June 1, 2017
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda Leo Alhamisi June 1, 2017
amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1 tayari kwa kuelekea
Mafia Mkoani Pwani.

Mwenge
wa Uhuru ni chombo kilichoasisiwa na baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni Tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa
huru la Tanganyika.

Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo  Mhe Paul C. makonda  amesema kuwa jumla ya
Miradi 40 imepitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2017 katika Mkoa wa
Dar es salaam yenye thamani ya Shilingi 244,392,530,334 huku akibainisha
kuwa Miradi 12 imezinduliwa, Miradi 15 imewekewa mawe ya Msingi, Miradi
miwili imefunguliwa na Miradi 11 imetembelewa.

Rc
Makonda alisema kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru tangu mwanzo zimekuwa
kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo , uzalendo, Umoja ,
Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya nchi.

Alisema
kuwa Mwenge wa Uhuru Mwaka 2017 wenye kauli mbiu isemayo Shiriki kukuza
uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu pia umebeba jumbe
mbalimbali ikiwemo kupiga Vita Maambukizi mapya ya UKIMWI na Malaria
sambamba na kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya.

Katika
mapambano dhidi ya Dawa za kulevya jitihada ya kudhibiti ni ajenda
muhimu kwa mustakabali wa maisha ya mtanzania kwa kuwa linagusa nguvu
kazi ya Taifa.

"Katika
kutimiza adhma iliyowekwa na waasisi wa Taifa la Tanzania wakati wa
kuanzisha Mbio za Mwenge kama kichocheo kikubwa katika kuhamasisha
Maendeleo, uzalendo, Umoja, Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje
ya Taifa letu, mkoa wetu wa Dar es salaam ulipokea Mwenge wa Uhuru siku
ya tarehe 25/05/2017 saa 3 asubuhi katika eneo la Kongowe Shule ya
Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma ukitokea Mkoa wa Lindi na
kukabidhiwa katika wilaya ya Temeke ambapo ndipo ulipoanza kukimbizwa"
Alisema Mhe Makonda

Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika Wilaya
zote za Mkoa wa Dar es salaam kuanzia Temeke, Kigamboni, Ilala,
Kinondoni na Ubungo  na kuzindua miradi mbali mbali ya kimaendeleo.

Mhe
Makonda amewashukuru wakazi wote wa Mkoa wa Dar es salaam kwa
kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru katika maeneo yote
ulipopita.

Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa Pwani Mhe Ernest Ndikilo amesema kuwa Mwenge
wa Uhuru ukiwa Mkoani Pwani utazuru katika Wilaya zote Saba zilizopo
katika Mkoa huo sambamba na kuzindua, Kutembelea, na kuweka Mawe ya
Msingi katika miradi mbalimbali.
Alisema Miradi hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru itagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni themanini na tano.

Mhe
Ndikilo alisema kuwa Mkoa wa Pwani una maendeo makubwa na ya kutosha
katika uwekezaji hususani uwekezaji wa Viwanda hivyo amewasihi wananchi
kwa umoja wao Kwenda  kuwekeza Mkoani Pwani

Mwaka
huu utakuwa mwaka wa 24 tangu mbio za Mwenge wa Uhuru zirejeshwe chini
ya utaratibu wa usimamizi wa serikali. Hii ilitokana na mabadiliko ya
kidemokrasia baada ya nchi  kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya
siasa mwaka 1992.