Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 11, 2017

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Akabidhi Mipira ya Maji Kwa Wananchi wa Kijiji cha Mwera Kiongoni

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akimkabidhi mipira ya maji Mmoja wa Wazee wa Kijiji cha Mwera Kiongoni kwa ajili ya kuunganisha maji kupata huduma hiyo katika kijiji chao. Mipira hiyo jumla ya roli sita zimetolewa na Mbunge na Mwakilishi wa jimbo hilo la Tunguu Zanzibar.Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said akiwa na wananchi wa Kijiji cha Mwera Kiongoni sehemu ya Jimbo lake wakiitikia dua baada ya kukabidhi mipira ya maji kwa ajili ya kijiji hicho kuweza kupata huduma hiyo. kwa wakazi wake.


Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said akisikiliza matatizo ya Wananchi wa Jimbo lake katika Kijiji cha Mwera Kiongoni Wilaya ya Kati Unguja akiwa na wananchi hao akipata changamoto zinazowakabili. baada ya kukabidhi mipira ya maji iliotolewa na Mwakilishi na Mbunge kwa Wananchi wa kijiji hicho kuunga maji.


Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akizungumza na Wananchi wa jimbo lake katika Kijiji cha Mwera Kiongoni Wilaya ya Kati Unguja alipofika kukabidhi mipira ya maji roli sita ili kuweza kupata huduma ya maji safi na salama.


Mwenyekiti wa Tawi la CCM Mwera Kiongoni akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa mipira ya maji kwa ajili yao kupata huduma hiyo.


Diwani wa Wadi ya Ubago akizungumza wakati wa hafla hiyo.


Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akimsikiliza Diwani wa Wadi ya Ubago akitowa maelezo ya upatikanaji wa maji hayo kwa wananchi wa kijiji cha mwera kiongoni. wanancc chi wa kijiji hicho walikuwa wakipata shida ya huduma hiyo muhimu kwa jamii.

Imetayarishwa na OthmanMapara.Blog.

Zanzinews.com.
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP