Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa rasmi wilaya ya Mkuranga ukitokea wilaya ya Rufiji huko mkoani Pwani na umetembelea miradi 11 ya Maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi billion 24.7.

Akizungumza wakati wa kubadhiwa mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Filibeto Sanga amesema miradi hiyo 11 iliyotembelewa ni pamoja na afya, elimu, kilimo na mradi wa ujasilia Mali kwa vijana.

Aidha katika miradi hiyo kumi na moja mwenge wa Uhuru umezindua miradi mitatu ambayo ni huduma ya upasuaji katika kituo cha afya Kilimahewa, kufungua nyumba za walimu katika shule ya sekondari Mkugilo pamoja na kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Mwanambaya wilayani humo.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 Amour Hamadi Amour ametoa wito kwa watanzania kuwa na uzalendo wa kuthamini vya kwao ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuifanya Tanzania ya viwanda.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa katika kuelekea nchi ya viwanda ni vyema Watanzania wakawa na utamaduni wa kutumia bidhaa za ndani ili kukuza uchumi wa nchi na taifa kwa ujimla.

Hata hivyo mbio hizo za mwenge wa Uhuru wilayani mkuranga mkoani Pwani zimeudhuriwa na watendaji mbalimbali wa Halmashauri hiyo akiwemo Mkurugenzi injinia Mshamu Munde na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Abeid.
 Mkuu wa Wilaya ya mkuranga, Filibeto Sanga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Njopeka waliojitokeza kuupokea mwenge wa uhuru,mwenge huo unatarajia kupitia miradi 11 ya maendeleo yenye thamani ya bilion 24.7 mkoani Pwani.
 Mkuu wa Wilaya ya mkuranga, Filibeto Sanga (kulia) akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Rufiji Juma Abdalah tayari kwaajili ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo.mkoani Pwani.
 Mganga mkuu Wilaya ya Mkuranga Dkt.Steven Mwandambo wa (kwanza kulia) akitoa maelekezo mbele  ya viongozi wengine ya namna chumba upasuaji kitakavyo saidia kinamama wajawazito kijiji cha kilomahewa.mkoani Pwani. 
 Kiongozi Mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour akizindua nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Mkugilo mkoani Pwani.
 Kiongozi Mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour akipanda mti katika shule ya Sekondari Mkugilo mkoani Pwani ikiwa  ni ishara ya kuhimiza wananchi kutunza na kuhifadhi mazingira,


 Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Abeid wa (kwanza kulia akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani wa Wilaya ya Mkuranga.