NHC
TANGA YAWATANGAZIA KIAMA WANAOGUSHI FOMU ZA UPANGISHAJI




 Meneja wa Shirika la
Taifa la Nyumba(NHC) mkoani Tanga Mussa Kamendu
katikati akionyesha moja kati ya chemba ambazo zinafanyiwa ukarabati
eneo la mtaa wa market Jijini Tanga  na Fundi Mchundo wa Shirika hilo
jana wakati alipotembelea kuona hali ya ukarabati huo
unavyoendelea

 Meneja wa Shirika la
Taifa la Nyumba(NHC) mkoani
Tanga Mussa Kamendu katikati akionyesha waandishi wa habari maeneo
mbalimbali waliokarabati
 Meneja wa Shirika la Taifa la
Nyumba(NHC) mkoani Tanga Mussa Kamendu katikati akionyesha waandishi wa
habari maeneo mbalimbali waliokarabati
Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba(NHC)
mkoani

Tanga Mussa Kamendu kulia akionyeshwa moja kati ya chemba ambazo
zinafanyiwa ukarabati eneo la mtaa wa market Jijini Tanga  na Fundi
Mchundo wa Shirika hilo wakati alipotembelea kuona hali ya ukarabati huo
unavyoendelea


 Meneja wa Shirika wa Shirika la
Taifa la Nyumba Mkoani Tanga (NHC),Mussa Kamendu akikagua ukarabati wa
nyumba za shirika hilo ambazo zinafanyiwa marekebisho


 Mafundi wakiendelea na
kazi kama wanavyoonekana


Meneja
wa Shirika wa Shirika la Taifa la Nyumba Mkoani Tanga (NHC),Mussa
Kamendu akikagua mitaro iliyochimbwa kwa ajili ya kupitisha mfumo wa
maji taka
SHIRIKA la Nyumba la Taifa Mkoani
Tanga (NHC) limewa tahadharisha watu wanaoghushi fomu za maombi ya
kupangisha katika nyumba zao na kuziuza kwa wananchi kuacha mara moja
tabia hiyo kwani watakabanika watachukuliwa hatua kali za kisheria
ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya dola.



Kauli hiyo ilitolewa juzi na Meneja wa Shirika hilo,Mussa Kamendu wakati
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu mipango
mbalimbali ya shirika hilo ikiwemo kuzifanyia ukarabati nyumba
wanazozimiliki ili ziweze kuwa katika muonekana mzuri kwa zile ambazo
zimeonekana  kuchakaa.



Alisema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wananchi kughusi fomu ambazo
zinatolewa na shirika hilo kwa kuzisambaza kwa wengine na kuwauzia jambo
ambalo ni kinyume na utaratibu uliopo.



“Ukiangalia sisi kama shirika tumekuwa tukitoa fomu kwa wananchi ambao
wanataka kupangisha kwenye nyumba zetu lakini katika hilo kumejitokeza
baadhi ya watu wanazitoa kopi na kuziuza kitendo ambacho ni uvunjifu wa
taratibu tulizoziweka “Alisema.



“Jambo hili ni hatari hasa kwa ustawi wa shirika letu kwani

linachangia kukosesha mapato hivyo tutahakikisha tunawa shughulikia
watakaobainika kufanya hivyo bila kuangalia nafasi yake kwa maslahi ya
ustawi wa shirika letu “Alisema Meneja huyo.



Aidha alisema licha ya jitihada hizo lakini pia wameweka mpango

kabambe wa kuhakikisha wadaiwa wote wanalipa madeni yao ya pango kwa
wakati ili kuweza kutoa fursa kwa shirika hilo kuweza kujiendesha na
kuweza kufanikisha mipango ya maendeleo.



Kamendu aliwataka pia wapangaji wao wazingatie mikataba walioingia na
shirika hilo ikiwa pamoja na utunzaji mazingira ya nyumba hizo na kulipa
kodi kwa wakati kabla ya hatua za kisheria hazijachukuliwa.



Aidha pia alisema hivi sasa tayari shirika hilo limekwisha anza

kufanya ukarabati wa nyumba hizo ikiwa pamoja na kuboresha mifumo ya
maji taka, kuweka bati mpya na upakaji wa rangi katika nyumba zilizopo
katika maeneo mbalimbali ndani ya Jiji la Tanga.



Alisema miongoni mwa nyumba walizoanza kuzifanyia ukarabati ni pamoja na
zilizopo maeneo ya Chumbageni,kwa karatunga,barabara 4,6,Bombo na
Raskazoni ambapo marekebisho hayo yanafanyika kwa lengo la kurudisha
ubora wa nyumba hizo.



Aliongeza kuwa marekebisho yanayofanywa na shirika hilo yana lengo la
kuhakikisha nyuma zao zinakuwa katika ubora mzuri ambao utamfanya
mpangaji aweze kuishi kila kukumbana na usumbufu wa aina
yeyote.
Habari kwa Hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha