Mkutano kati ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na rais wa Togo Faure Gnassingbé, ulilazimika kupangwa upya baada ya mvutano uliotokea kati ya walinzi wa viongozi hao.
Mtandao wa Times of Israel ulisema kuwa mvutano huo ulitokea wakati walinzi wa Israel walikataa kuwaruhusu walinzi wa Togo kuingia mkutano ambapo viongozi hao walikuwa wakutane mjini Monrovia nchini Liberia.
Bwana Gnassingbe na Netanyahu walikuwa wanahudhuria mkutano wa Jumuiya ya nchi za Afrika magharibi (Ecowas).
Hata hivyo bwana Netanyahu alitaja kuwepo kwake kama wa kihistoria
"Hii ndiyo mara ya kwanza Ecowas kumualika kiongozi kutoka nje ya Afrika kuwahutubia. Ninatoa shukran zangu nyingi. Israel imerudi Afrika kwa njia kubwa, Netanyahu alinukuliwa akisema na gazeti la Jurusalem Post.
|
0 Comments