Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 21, 2017

Majaliwa aongoza wananchi wa Mbeya kumzika Linah Mwakyembe

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na mkewe Marry Majaliwa wakishirikiana kuweka shada la maua katika kaburi la Linah Mwakyembe wilayani Kyela mkoani Mbeya

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wakazi wa Kyela hususani wa Kijiji cha Ikolo mkoani Mbeya katika mazishi ya Linah Mwakyembe ambaye ni Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.

Linah alifariki Julai 15 mwaka huu katika Hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akitibiwa maradhi ya Saratani ya matiti na kuzikwa jana kijijini kwao Ikolo, Kyela mkoani Mbeya.
Waziri Mkuu Majaliwa, aliambatana na mkewe, Mary Majaliwa,lakini pia katika mazishi hayo walihudhuria, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa, wakuu wa idara mbalimbali za chama na serikali.
Spika wa Bunge, Job Ndugai na Naibu wake Dk. Tulia Ackson pia ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo. Waziri Mkuu Mstaafu, John Samwel Malekela na Mkewe, Anne Kilango Malecela pia walihudhuria mazishi hayo yaliyomalizika muda si mrefu.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP