Marufuku ya laptopu ndani ya ndege zinazofanya safari ya moja kwa moja kutoka nchini Saudi Arabia hadi Marekani imeondolewa, kwa mujibu wa shirika la ndege la Saudi Arabian.
Linasema kuwa viwanja vya ndege ambavyo ndege zinazoelekea Marekani hutumia, vimeruhusiwa na idara ya ulinzi ya Marekani.

Uwanja wa King Khalid mjini Riyadh ndio wa mwisho kati ya viwanja kumi vilivyoondolewa marufuku hiyo.
Mwezi Machi Marekani ilipiga marufuku laptopu na vifaa vingine vikubwa vya elektroniki kutoka nchi nane za kiislamu.
Viwanja wa King Abdulaziz mjini Jeddah na King Khalid mjini Riyadh vyote vimekaguliwa na kuruhusiwa laptopu kuingia viwanjani humo.
Viwanja hivyo viwili vinatumiwa na ndge zinazosafiri moja kwa moja kutoka Saudi Arabia kwende Marekani.
Shirika la ndege la Saudi Arabian ambalo pia linajulikana kama Saudia ndilo pekee ambalo hufanya safari za moja kwa moja kuenda Marekani.