Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 5, 2017

MANISPAA YA UBUNGO YAANZISHA REJESTA YA WAKAZI KWA KILA MTAA


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akionyesha kitabu cha kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananchi katika Ofisi za serikali muda mchache mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kibamba CCM. Leo June 5, 2017

 Mfano wa Fomu ya huduma kwa mwananchi (Fomu ya malalamiko)

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa kuelezea dhima ya kuanzisha Daftari la wakazi wa kila Mtaa katika Manispaa ya Ubungo.Leo June 5, 2017


 Kitabu cha Kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananchi katika ofisi za serikaliMkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa
kuelezea dhima ya kuanzisha Daftari la wakazi wa kila Mtaa katika
Manispaa ya Ubungo.
Leo June 5, 2017 Mfano wa Fomu ya Rejista ya Wakazi katika kila MtaaIli kupunguza uhalifu katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam imebainika kuwa ni vyema kuwatambua wananchi wote na mahali wanapoishi
ikiwemo kubaini wageni wote wanaowasili katika Manispaa ya Ubungo ikiwa ni pamoja na mahali wanapofikia.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kibamba Chama Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Kayombo amesema kuwa  kumekuwa na uhalifu kwa kiasi kikubwa katika maeneo mbalimbali Katika Manispaa hiyo jambo ambalo limetafutiwa muarobaini kwa kuanzishwa daftari la wakazi litakalobainisha wakazi wote ili kukitokea uhalifu iwe rahisi kuwabaini wahalifu hao.
Kuanzishwa kwa Daftari la Rejesta ya Wakazi wa Mtaa ni agizo lililotolewa hivi karibuni na MKUU
wa Wilaya ya Temeke Mhe
Felix Lyaviva
kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa za
Kigamboni, Ilala, Temeke, Kinondoni na Ubungo
wakati akihutubia kwa niaba
ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda katika ufunguzi wa semina ya
mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ili kuwaelimisha watumiaji wa Intaneti wapatao
milioni 20 sambamba na watumiaji wa simu za mikononi wapatao milioni 40 kuwa na
matumizi bora ya simu za mikononi na mitandao ya kijamii.


Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amesema kuwa pamoja na kuanzishwa kwa Daftari la Rejesta ya wakazi wa Mtaa pia kutakuwa na Fomu ya Rufaa ya Malalamiko katika kila Mtaa sambamba na kitabu cha kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananchi katika Ofisi za serikali.


Tayari vitabu hivyo vyote vimeanza kugawanywa katika kila Mtaa ili kuanza utekelezaji wa zoezi hilo haraka iwezekanavyo.IMETOLEWA NA:

KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO 

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP