Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 20, 2017

Rais Trump akutana na wabunge wa chama chake

Wamarekani wakipata huduma kupitia ObamaCareHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWamarekani wakipata huduma kupitia ObamaCare
Rais Donald Trump amekutana na maseneta wote 52 wa chama chake cha Republican na kuwataka kuupatia nguvu mpango wake ili uweze kuifuta sheria iliyo kuwepo ya huduma ya afya maarufu kama ObamaCare.

Rais huyo wa Marekani amewataka watunga sheria hao kutoondoka kwenda likizo ya mwezi wa Nane hadi pale watakapokubaliana mpango wa huduma ya afya ambao utaweza kupitishwa na mabunge yote mawili ya nchi hiyo.
Wiki hii Rais Trump amekuwa akihaha baada ya wabunge wanne wa chama chake kusema kwamba hawataunga mkono muswada mpya wa sheria ambao unatarajiwa kuchukua nafasi ya ObamaCare.
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP