Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 1, 2017

Waliobadili jinsia kuajiriwa na jeshi mwaka ujao Marekani

Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis{pichani juu} amechelewesha kuidhinishwa kwa mpango wa rais Obama wa watu waliobadili jinsia kujiunga na jeshi la Marekani.

Sera hiyo mpya itakayowaruhusu wanajeshi kubadili jinsia huku wakiendelea kuhudumu na kuweka viwango vya matibabu sasa itaanza kutekelezwa mnamo mwezi Januari 1 2018.
Maafisa wa Pentagon wanasema kuwa huduma tofauti hazijakubaliana kuhusu ni lini kuwakubali walioajiriwa.
Wanaharakati wanasema kuwa hawafurahishwi na kucheleweshwa huko
Mwanamume aliyebadilisha jinsia yake na kuwa mwanamke
Image captionMwanamume aliyebadilisha jinsia yake na kuwa mwanamke
''Kila siku inayopita bila sera hiyo inazuia uwezo wa jeshi wa kuwasajili wanajeshi wazuri na werevu bila kujali jinsia'', ,alisema msemaji wa shirika la haki za kibinaadamu Stephen Peters.
Katika taarifa Bwana Mattis alisema katika barua ilionukuliwa na gazeti la Washington post kwamba ameamua muda zaidi unahitajika kufanya uamuzi baada ya kushauriana na maafisa wa ulinzi.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP