Mtu aliyejitoa mhanga ameua takriban watu 27 kaskazini mashariki mwa Nigeria na kujeruhi wengine zaidi ya wanane.
Vyombo vya usalama katika eneo hilo vimesema, watu watatu waliojitoa mhanga akiwemo mwanamke mmoja, walijilipuwa wenyewe kwenye lango la kuingilia kambi ya wakimbizi.

Shamabulio hilo lilitokea karibu na mji wa Maiduguri katika jimbo la Borno, eneo ambalo ni ngome ya kundi lenye itikadi kali la Boko Haramu.
Karibu watu mia moja hamisini wameuawa katika mashambulio yanayodaiwa kufanywa na wapiganaji toka kuanza kwa mwezi wa Sita.
Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa Jumatatu na watafiti wa Kimarekani wanaopinga ugaidi, Boko haramu wamekuwa wakitumia wanawake na wasichana zaidi kufanya mashambulio kushinda wapiganaji wengine katika historia.