Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria{Pichani} amemfukuza kazi waziri wake mkuu Abdelmadjid Tebboune, ambaye aliteuliwa katika nafasi hiyo miezi isiyozidi mitatu.
Hakuna sababu zilizotajwa za kuondolewa kwake kazini.

Lakini hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya Rais kumtumia barua kali bwana Tebboune kutaka mabadiliko ya sera.
Tayari waziri mkuu mpya ametajwa kuwa ni Ahmed Ouyahia ambaye alikuwa mnadhimu mkuu wa Rais.