Mgeni rasmi Waziri wa Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge Akisisitiza jambo mara baada ya
kutembelea Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya wakulima (Nanenane)
ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Mgeni rasmi Waziri wa Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge akisalimiana na Afisa habari wa Wizara
ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Ndg Issa Sabuni mara baada ya kutembelea Maonesho ya
wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani
Lindi.
Mgeni rasmi Waziri wa Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Maonesho ya
wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani
Lindi.
Mgeni rasmi Waziri wa Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge akipata ufafanuzi kuhusuidara ya uzalishaji wa mifugo na masoko inavyofanya kazi mara baada ya kutembelea Maonesho ya
wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani
Lindi.

Mgeni rasmi Waziri wa Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge akipata ufafanuzi kuhusuidara ya
uzalishaji wa mifugo na masoko inavyofanya kazi mara baada ya kutembelea
Maonesho ya
wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo
Mkoani

na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge akipata ufafanuzi kuhusuchangamoto za masoko ya bidhaa zinazotengenezwa kwa ngozi kutoka kwa meneja wa Robi Leather Product Bi Rose Otieno mara baada ya kutembelea
Maonesho ya
wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo
Mkoani
Lindi.

Mgeni rasmi Waziri wa Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge alipowasili kwenye
Maonesho ya
wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo
Mkoani
Lindi.

Na Mathias Canal, Lindi

Waziri wa Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge ameipongeza Wizara ya Kilimo Mifugo na
Uvuvi kwa elimu wanayoitoa kwa wananchi kuhusu utunzaji wa malisho ambayo ni
nyasi na mikunde kwa ajili ya mifugo kwani jambo hilo litawawezesha wananchi
kuwa na mifugo yenye afya bora.

Mhandisi Lwenge ameyasema hayo
alipotembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi idara ya uzalishaji wa
mifugo na masoko wakati wa Maonesho ya wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa
yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Alisema kuwa malisho ni chakula cha
msingi cha mifugo ambacho kinajumuisha aina mbalimbali za nyasi na mikunde.

Pamoja na kutolewa elimu juu ya
umuhimu wa utunzaji wa malisho lakini pia amesisiza zaidi wizara ya kilimo
kutoa elimu kuhusu utunzaji wa malisho hayo jambo ambalo litawawezesha wafugaji
kuipatia mifugo yao chakula bora na cha kutosha wakati wote.

Zipo faida nyingi za kupanda
malisho ikiwa ni pamoja na kurahisisha upatikanaji wa chakula cha mifugo chenye
viini lishe kama wanga, protini madini na vitamin.

Faida Zingine ni kurutubisha ardhi
hasa malisho aina ya mikunde sambamba na kuzuia mmomonyoko wa ardhi.

Mhandisi Lwenge amesema kuwa malisho ndio chakula
kikuu cha mifugo inayochengua (Ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda na ngamia.

MWISHO