Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali
ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya
Ngongo Mkoani Lindi. (Picha zote na Mathias Canal)



Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe
akizungumza jambo wakati akitembelea mabanda
mbalimbali
ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja
vya
Ngongo Mkoani Lindi.


Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe alipotembelea kitalu cha Mikorosho wakati wa  Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja
vya
Ngongo Mkoani Lindi.


Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda
la Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa kilimo cha Ukanda wa Tropiki (IITA) wakati wa Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja
vya
Ngongo Mkoani Lindi.


Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe
akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda
la Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa kilimo cha Ukanda wa Tropiki
(IITA) wakati wa Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika
katika viwanja
vya
Ngongo Mkoani Lindi.


Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe
alipotembelea mashamba darasa ya mazao mbalimbali wakati wa  Maonesho ya Wakulima
(Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja
vya
Ngongo Mkoani Lindi.


Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe
alipotembelea mashamba darasa ya mazao mbalimbali wakati wa  Maonesho ya Wakulima
(Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja
vya
Ngongo Mkoani Lindi.


Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe
alipotembelea shamba darasa la mikorosho wakati wa  Maonesho ya Wakulima
(Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja
vya
Ngongo Mkoani Lindi.

Na Mathias
Canal, Lindi




SHEREHE za wakulima maarufu kama Nane Nane zimetajwa kuwa ni darasa huru kwa
wakulima, wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla kwani zinatoa nafasi kwao
kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kilimo chenye tija, Ufugaji wa kisasa na
Uvuvi wenye tija pasina kuharibu rasilimali za serikali.

Hayo
yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi
Methew J. Mtigumwe wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa
yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.



Alisema
kuwa serikali inatambua kadhia inayowakabili wakulima nchini ikiwemo pembejeo
feki ambazo wakulima wanauziwa, hivyo kupata hasara ikiwamo mazao kidogo na
hafifu tofauti na kusudio lao la kujipatia mazao mengi ya biashara na chakula
jambo ambalo inalifanyia kazi ili kukabiliana nalo kwa haraka.


Maonyesho haya Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
yatawasaidia wakulima kupata elimu juu ya pembejeo halisi ikiwamo mbegu, dawa
(viuatilifu), mbolea kutoka kwa mashirika husika yanayozalisha pembejeo mbali
mbali, ili kuwasaidia kuepuka kununua pembejeo feki ambazo huwasababishia
hasara na kuwakatisha tamaa.


Sherehe hizi huambatana na maonyesho ya bidhaa za kilimo yanayofanywa na
wakulima na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya kilimo, lengo
likiwa ni kujitangaza shughuli zao, kubadilishana uzoefu na wataalamu wa
kilimo.


Pia wakulima wadogo ambao ni wengi ukilinganisha na wakulima wakubwa
watajifunza mbinu mpya za kitaalamu za kilimo zinazoendana na wakati uliopo kwa
maana ya mabadiliko ya kiteknolojia na tabia nchi ili wakulima waweze kulima
kilimo cha kisasa na kunufaika kiuchumi.


Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa Kwa muda mrefu wakulima wamekuwa wakilima kilimo
cha mazoea ambacho hakizingatii kanuni za kitaalamu, jambo lililowasababisha
kukata tamaa na kuona kuwa kilimo hakilipi kutokana na mbinu duni
walizozitumia.


Alisema kuwa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi inajipambanua zaidi kumkwamua
mkulima ili Wakulima nchini waondokane na kilimo cha kubahatisha cha kutegemea
mvua na badala yake wajikite katika kilimo cha umwagiliaji ambacho ni cha
uhakika, kinachoweza kuyabadilisha maisha yao kiuchumi kutokana na mazao mengi watakayopata.


"Natambua kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanategemea sekta ya
kilimo kama ajira yao Sehemu kubwa ya kilimo ni cha wakulima wadogo wadogo
ambao mashamba yao yana ukubwa wa hekta 0.9 na hekta 3.0 kwa kila moja, Karibu
asilimia 70 ya ardhi ya kilimo na mazao inalimwa kwa kutumia jembe la mkono,
asilimia 20 hutumia maksai na asilimia 10 hutumia trekta Hivyo kama wizara
tutajitahidi kadri iwezekanavyo kuwakwamua wananchi ili kuondokana na uduni
katika mavuno" Alisema Mtigumwe


Mbali na hayo, kilimo cha Tanzania ni cha kutegemea mvua, uzalishaji wa mazao
ya chakula ndio unaongoza katika uchumi wa kilimo. Hekta milioni 5.1 zinalimwa
nchi nzima kila mwaka, kati ya hizo asilimia 85 ni kwa ajili ya mazao ya
chakula tu, na wanawake ndio wafanyakazi wakubwa mashambani.
Mhandisi
Mtigumwe anasema katika maonesho hayo anatarajia wakulima watajifunza mbinu
bora na za kisasa za kilimo zitakazowawezesha kupata mazao mengi na kuinua
kipato chao.


Aidha ametoa  wito kwa wakulima na
mashirika kujitokeza katika maonesho hayo kwa sababu watapata fursa ya
kujifunza mambo mengi na kubadilishana uzoefu na wataalamu mbalimbali wa
kilimo.

MWISHO