Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Aug 10, 2017

Paul Kagame ashinda asilimia 98.78 ya kura

Rais wa Rwanda Paul Kagame amethibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa wiki iliopita na tume ya uchaguzi nchini humo kulingana na chombo cha habari cha AFP.

AFP imeripoti kwamba tume hiyo ilimuongezea rais Kagame asilimia ya kura alizopata kutoka 98.63, ikiwa ni takwimu zilizotangazwa hapo awali hadi asilimia 98.79.
Alikabiliana na wapinzani wawili , ambapo hakuna hata mmoja wao aliyefanikiwa kupata asilimia moja ya kura.Rais huyo amekuwa madarakani tangu 2000 na amekosolewa kwa unyanyasaji wa haki za kibinaadamu.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP