Kuhesabu kura Mombasa
Image captionKura zinaendelea kuhesabiwa katika vituo vingi

Kura zinaendelea kuhesabiwa na matokeo kutangazwa baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Kenya Jumanne.
Katika matokeo yaliyokuwa yametangazwa kufikia saa kumi alfajiri, Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee alikuwa akiongoza akiwa na kura 6,574,087 (55.21%) akifuatwa na Raila Odinga wa muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) aliyekuwa na kura 5,236,724 (43.98%) Matokeo hayo ni ya vituo 31947 kati ya 40,883.
Kura ambazo zilikuwa zimeharibika kufikia wakati huo ni 307,252.
Katika baadhi ya vituo, shughuli ya upigaji kura ilichelewa kuanza na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) iliongeza muda kufikia wakati uliokuwa umepotezwa kabla ya kufungua vituo.
Kisheria, vituo vilitakiwa kufunguliwa saa kumi na mbili asubuhi na kufungwa saa kumi na moja jioni saa za Afrika Mashariki.
Lakini katika baadhi ya maeneo, mvua kubwa ilitatiza uchukuzi na upigaji kura na kwingine hitilafu za kimitambo zikachangia kukwamisha upigaji kura. Muda wa kufungwa kwa vituo uliongezwa kwa vituo vilivyochelewa kufunguliwa.
Wengi wanahofia uwezekano wa kutokea tena kwa ghasia za baada ya uchaguzi sawa na ilivyotokewa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Watu zaidi ya 1,100 walifariki na wengine 600,000 kuachwa bila makao.

Tume ya uchaguzi imetangaza matokeo kutoka kwa vituo 31947 kati ya jumla ya vituo 40883 ambapo:

  • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 6,574,087 (55.21%)
  • Raila Odinga wa ODM kura 5236724 (43.98%)
  • Joseph Nyagah (huru) 29163 (0.24%)
  • Abduba Dida wa ARK 23318 (0.2%)
  • Ekuru Aukot wa Thirdway Alliance 20700 (0.17%)
  • Japheth Kaluyu (huru) 8806 (0.07%)
  • Cyrus Jirongo wa UDP 8521 (0.07%)
  • Michael Wainaina (huru) 6519 (0.05%)
Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 307,252
Ili kushinda, mgombea urais anahitajika kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa, na angalau asilimia 25 katika kaunti 24 kati ya kaunti 47 nchini humo.
Iwapo hakuna mgombea atakayetimiza hilo, basi uchaguzi wa marudio utafanyika katika kipindi cha siku 30.

Kujitokeza mapema

Wapiga kura walianza kujitokeza alfajiri na mapema kupiga kura.
Foleni ndefu zilishuhudiwa katika vituo vingi, na kwingine visa vya watu kuumia katika mkurupuko wa kupanga foleni vituo vilipofunguliwa viliripotiwa.

NairobiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWatu walianza kupanga foleni nje ya vituo mapema

Katika baadhi ya vituo, kuliripotiwa pia visa vya mitambo ya kuwatambua wapiga kura kufeli.
Katika moja kati ya vituo vinne nchini humo, maafisa wa IEBC walikuwa wamesema kwamba hakuna huduma nzuri ya mtandao maana kwamba wasimamizi wa uchaguzi katika vituo hivyo watahitaji kusafiri hadi ameneo yenye huduma nzuri ya simu kutuma matokeo kikamilifu.
Kumekuwa pia na taarifa kwmaba mwanamume mmoja ameuawa katika makabiliano kati ya wafuasi wa wagombea wawili katika kaunti ya Kilifi, pwani ya Kenya.
Lakini kulikuwa na kisa cha kutia moyo pale mwanamke mmoja alipojifunzua mtoto msichana alipokuwa kwenye foleni akijiandaa kupiga kura Pokot Magharibi.
Pauline Chemanang alisema kujifungua kwake ni baraka na akampa mtoto wake jina Kura, kwa mujibu wa kituo kimoja cha redio.

Isinya, Kajiado, Nairobi, Kenya, 08 August 2017.Haki miliki ya pichaEPA
Image captionMaafisa wa uchaguzi wanaendelea kuhesabu kura
Uhuru Kenyatta GatunduHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBw Kenyatta amewahimiza Wakenya kudumisha umoja
Raila OdingaHaki miliki ya pichaEPA
Image captionOdinga amesema anahofia kwamba huenda kukatokea wizi wa kura
Naibu Rais William Ruto akipiga kura katika kituo cha Kosachei, katika kaunti ya Uasin Gishu magharibi mwa Kenya
Image captionNaibu Rais William Ruto akipiga kura katika kituo cha Kosachei, katika kaunti ya Uasin Gishu magharibi mwa Kenya

Rais Kenyatta, baada ya kupiga kura yake kituo cha Mutomo eneo lake la nyumbani la Gatundu, kaskazini mwa Nairobi, alisema kwamba yuko tayari kukubali matokeo ya uchaguzi huo.
"Kwa wapinzani wangu, kama nilivyosema mara nyingi awali, ikitokea kwamba washindwe, basi hebu tukubali uamuzi wa wananchi. Nina nia, mwenyewe, kukubali nia ya wananchi," amesema.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alipiga kura yake katika mtaa wa Kibera, Nairobi.
Akiongea nje ya kituo hicho, aliwahimiza wafuasi wake: "Hebu tujitokeze kwa wingi na tupige kura."



Suti ya vipande sita na uchaguzi nchini Kenya
line break

Mwangalizi mkuu wa Umoja wa Ulaya Marietje Schaake amesema itategemea sana imani ya wananchi katika mfumo mpya wa kiteknolojia wa kupiga kura.
Kabla ya siku ya uchaguzi, meneja wa masuala ya teknolojia katika IEBC Chris Msando aliuawa na watu wasiojulikana.
Kulikuwepo na madai ya kwamba huenda kukawa na wizi wa kura na pia katika baadhi ya maeneo taarifa za kueneza kwa karatasi zenye ujumbe wa chuki zilizagaa.
Siku chache kabla ya uchaguzi, Wakenya wengi walikuwa wakinunua chakula na maji na kujihifadhia wakihofia hali baada ya uchaguzi.
Polisi pia walifanya mipango ya kushughulikia dharura iwapo ghasia zingetokea.

Wapiga kura kwenye foleni kaunti ya Uasin Gishu magharibi mwa Kenya
Image captionWapiga kura kwenye foleni kaunti ya Uasin Gishu magharibi mwa Kenya
GatunduHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWapiga kura wakiwa kwenye foleni eneo la Gatundu