Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa na viongozi kutoka mfuko wa pensheni wa PPF wakiwa katika Ardhi ya Hospitali ya halmashauri ya Mji wa Mafinga wakati wa kukabidhi vifaa tiba vyenye dhamani ya shilingi million sits.
 Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa Sambamba n Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga wakati wa kupokea msaada huu mkubwa wa vifaa tiba kutoka PPF
Baadhi ya madiwani na viongozi wa halmashauri ya Mafinga Mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupokea msaada wa vifaa Tiba vyenye thamani ya shilingi million sita kutoka mfuko wa pensheni wa PPF

Na fredy Mgunda, Iringa

Mfuko wa pensheni wa PPF umetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni sita katika hospitali ya halmashauri ya mji wa mafinga mkoani iringa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo afisa mawasiliano kutoka PPF Lulu Mengele alisema kuwa msadaa huo ni muendelezo wa kurudisha huduma kwa wananchi kwa kile wanachochangia kwenye mfuko huo.

"Wananchi ambao wamekuwa wadau wetu wakubwa wamekuwa wakichangia katika mfuko wetu kitu kichosababisha turudishe fadhila kwa kuleta maendeleo ya moja kwa moja kwa wananchi hasa katika maeneo ambayo serikali imezidiwa na ukiangalia maeneo ya afya ndio imekuwa changamoto kubwa kwa serikali ndio maana tumeanzia huku ili kuisaidia serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr John pombe Magufuli"alisema Mengele

Aidha Mengele aliwataka wananchi kujiunga katika mfuko huo wa pensheni ambao umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi hasa kwenye huduma ya afya kwa kuwa bima zao ni za bei nafuu lakini unatibu unachostahili kutokana na bima yako hivyo naomba muendelee kujiunga kwenye mfuko wa PPF kwa usalama wa maisha yenu.

"Ukitoa elfu ishirini tu inakusaidia kupata hudumu nzuri za afya hivyo naomba mjiunge na mfuko huu kwa kuwa ni msaada mkubwa sana kwenu hasa hapa Mafinga ambako kunashughuli nyingi za kijamii ambazo ni hatarishi kwa maisha yenu" alisema Mengele

Naye katibu wa hospitali ya mafinga Bernard Makupa ameshukuru msaada huo wa vifaa tiba kutoka PPF kwa kuwa vifaa hivyo vitakuwa Masada kwa hospitali.

"Tulikuwa na changamoto katika wodi za wazazi nilikuwa na upungufu mkubwa wa vitanda pamoja na magodoro yake hivyo kupata msaada huu unatusaidia kupunguza changamoto hivyo hivyo nawashukuru na kuwapongeza sana PPF kwa kurudi na kutoa huduma kwa jamii husika"alisema Makupa.

Mbunge wa jimbo la mafinga COSATO CHUMI amewashukuru PPF kwa msaada wa vifaa tiba ambavyo vitaendelea kupunguza changamoto zilizopo katika hospitali hivyo.

"Vifaa hivi vya Tiba ni muhimu sana katika idara yetu ya afya kwa kuwa inatupunguzia changamoto kwa wananchi wa wilaya ya Mufindi na mikoa ya Jirani wanayoitumia hospitali yetu ya Mafinga" alisema Chumi

Chumi aliwataka wananchi wa Mafinga Mjini kujiunga na mfuko huo wa pensheni kwa kuwa unamanufaa mengi sana hasa upande wa afya na ni muhimu kuwa na bimaa ya afya ya PPF kwa kuwa hudama yao ni ya ukahika na salama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga aliwashukuru mfuko wa pensheni wa PPF na mbunge Cosato Chumi kwa msaada huu mkubwa ambao kama halmashauri ingekuwa vigumu kutekeleza kutokana halmashauri hiyo kuwa Mpya.

"Chumi amekuwa mpambanaji mkubwa wa halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa kuleta maendeleo katika idara mbalimbali hivyo tunakuomba uendelee kutusaidia kutatua changamoto za halmashauri hii"alisema Makoga