MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NOTI BANDIA WILAYANI ILEMELA.
KWAMBA TAREHE 01.08.2017 MAJIRA YA SAA 23:00HRS KATIKA BAR IITWAYO THE DREAMS ILIYOPO MTAA WA KONA YA BWIRU KATA YA KITANGIRI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA RYOBA MANGULE, MIAKA 27, MKAZI WA IBUNGILO, AKIWA NA NOTI BANDIA SITA (6) ZA SHILINGI ELFU KUMI ZENYE THAMANI YA TSHS 60,000/=, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA.
AWALI ASKARI WALIPATA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA KATIKA MAENEO TAJWA HAPO JUU YUPO MTU MWENYE NOTI BANDIA. AIDHA BAADA YA KUPOKEA TAARIFA HIYO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI HADI ENEO HILO NA KUFANYA MSAKO MAENEO HAYO KISHA BAADAE WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA AKIWA NA KIASI HICHO CHA NOTI BANDIA.
POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, AIDHA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WANAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI NA USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA BADO UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWAOMBA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA. PIA ANAWATAKA VIJANA KUACHA TABIA YA UTENGENEZAJI NA USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA KWANI NI KOSA LA JINAI NA ENDAPO MTU ATAKAMATWA AKIWA ANAJIHUSISHA NA UHALIFU WA AINA HIYO HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA. |
0 Comments