Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Aug 12, 2017

Rais wa Misri Abdel Fattah El, kuingia nchini Jumatatu wiki ijayo

Rais wa Misri Abdel Fattah El anatarajiwa kuingia Nchini siku ya Jumatatu ya wiki ijayo kwaajili ya ziara ya siku mbili ambapo ataongozana na ujumbe wake na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Dr. John Magufuli.

Kutokana na ugeni huo mzito Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda amewataka wakazi wa jiji la Dar es salaam ikiwemo wenye Hotel, Magari na Migahawa kuchangamkia fursa ya ugeni huo katika kufanya biashara ili kujipatia kipato na kukuza Biashara zao.
Makonda amewataka wakazi wa Dar es salaam kuonyesha ukarimu tangu Rais atakapowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere hadi hapo atakaporejea nchini Misri siku ya Jumanne. Ugeni huu ni matunda ya uwezo wa Rais Magufuli katika kujenga mahusiano mazuri baina ya Tanzania na Mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP