Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Aug 9, 2017

Real Madrid walaza Manchester United 2-1 Kombe la Super Cup Uefa

Isco asherehekea dhidi ya Manchester UnitedHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIsco amefunga mabao 10 katika mashindano yote mwaka 2017
Manchester United walizidiwa nguvu na mabingwa wa Uhispania na Ulaya Real Madrid kwenye mechi ya Kombe la Super Cup la Uefa iliyochezewa Skopje, Macedonia chini ya joto kali.
Madrid walidhibiti mchezo huo kuanzia kipenga cha kwanza kilichopulizwa.

Walijipata kifua mbele pale Casemiro alipowafungia, muda mfupi baada ya kugonga mwamba wa goli.
Waliongeza la pili kupitia Isco aliyefunga akiwa hatua nane kutoka kwenye goli baada ya kubadilishana pasi na Gareth Bale, ambaye alichezeshwa safu ya mashambulizi badala ya Cristiano Ronaldo.
Mshambuliaji wa United aliyenunuliwa £75m Romelu Lukaku alikomboa bao moja lakini Marcus Rashford akapoteza fursa nzuri ya kufunga kwa kuutuma mpira nje.
Madrid wamekuwa timu ya kwanza kufanikiwa kutetea Kombe la Super Cup la Uefa tangu 1990.
Mechi hiyo ilichezewa katika uwanja chini ya joto kali la nyuzi joto 30C katika mji mkuu huo wa Macedonia.
Wachezaji walipewa muda mara mbili kupoesha joto, kama chini ya utaratibu wa Uefa.
Red Devils wametumia £146m majira ya joto kununua mshambuliaji wa Everton Lukaku (£75m), kiungo wa kati wa Chelsea Nemanja Matic (£40m) na beki wa Benfica Victor Lindelof (£31m) wakijaribu kujiimarisha baada ya kumaliza nambari sita ligini msimu uliopita.
Wachezaji hao watatu walichezeshwa na meneja Jose Mourinho dhidi ya Madrid.
Cristiano RonaldoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionCristiano Ronaldo aliingia nafasi ya Karim Benzema baada ya dakika 83
Upande wa Madrid, ni Ronaldo pekee ambaye alikuwa hayupo kwenye kikosi kilichoanza mechi ukilinganisha na kikosi kilichocheza fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Juventus.
United walihangaika dhidi ya Madrid, hasa kipindi cha kwanza ambapo Madrid walitawala kwa kasi na pasi.
Real Madrid walilaza Manchester United katika kombe la Super CupHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMourinho alitumia vipindi vya mapumziko ya kutuliza joto kuwashauri wachezaji wake
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP