Mfalme Salman bin Abdul Aziz al-SaudHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionMfalme Salman bin Abdul Aziz al-Saud
Mamia ya watu wanaarifiwa kutoroka katika eneo la mashariki mwa Saudi Arabia baada ya mapigano ya wiki kadhaa kati ya vikosi vya usalama na watu waliojihami.
Ni kisa cha hivi karibuni cha kukithiri kwa ghasia katika jimbo la mashariki, za waumini wa madhehebu ya Shia wanaodai haki zaidi.

Mji wa Awamiya ni nyumbani anakotoka Sheikh Nimr al-Nimr -- kiongozi wa kidini mwenye ushawishi anayewaunga mkono waandamanaji wa Shia, ambaye aliuawa mwaka mmoja na nusu uliopita.
Katika wiki za hivi karibuni, ghasia katika eneo hilo zinaonekana kuchukua sura mpya na ya hatari zaidi.
Vikosi vya usalama vimelenga maeneo ya kale ya Awamiya, ambayo wanasema ni sehemu wanakojificha wapiganaji wa Shia.
Maafisa wa utawala wanataka kulibomoa eneo hilo la kale lenye miaka 200 katika operesheni ilioanzishwa mnamo mwezi Mei.
Maafisa kadhaa wa polisi na wanaume waliojihami wameuawa katika mpigano ya hivi karibuni.
Sasa wakaazi wanatoroka ghasia hizo-- wanaharakati katika eneo hilo wanasema vikosi vya usalama vinajaribu kuwatimua.