Aliyekuwa waziri wa ugatuzi nchini Kenya Anne Waiguru
Image captionAliyekuwa waziri wa ugatuzi nchini Kenya Anne Waiguru
Aliyekuwa waziri wa ardhi nchini Kenya Charity Ngilu ni miongoni mwa wanawake watatu nchini Kenya wanaotarajiwa kuwa magavana wapya wa kaunti zao.
Ngilu ambaye aliwania wadhfa huo katika kaunti ya Kitui nchini Kenya kupitia chama cha Narc alimshinda Gavana Julius Malombe kwa wingi wa kura.

Mgombea mwengine mwanamke ambaye ameshinda wadhfa wa Ugavana ni aliyekuwa naibu wa spika bungeni Dkt Joyce Laboso .
Laboso amemshinda gavana Isaac Rutto ambaye ni miongoni mwa viongozi wakuu wa muungano wa upinzani Nasa.
Mwanamke huyo ambaye alikuwa akigombea wadhfa huo kupitia chama tawala cha Jubilee alikuwa ameshutumiwa na mpinzani wake aliyemtaka kuwania ubunge katika eneo la Nyanza alikoolewa.
Mgombea mwengine ni Anne Waiguru ambaye wakati mmoja alihudumu kama waziri wa maswala ya ugatuzi .
Waiguru ambaye alilazimika kujiuzulu katika wadhfa huo kutokana na madai ya ufisadi yaliomkabili anaendelea kupata ushindi dhidi ya Martha Karua aliyewahi wakati mmoja kugombea urais mbali na kuwa waziri..
''Nafurahi sana, watu wa Kirinyaga wanafurahi'', alisema huku kukiwa na pongezi na shangwe kutoka kwa wafuasi wake.
Ni miongoni mwa wanawake watatu ambao wanatarajiwa kuwa magavana na anasema kuwa safari yake fupi imekuwa ngumu.
''Imekuwa ngumu , ngumu sana, sijui ni mara ngapi nilitaka kujiondoa lakini nikaamua kusalia kwenye kinyanganyiro cha kuwania wadhfa huu''.
Anasema ushindi wake umetoa mfano wa mtoto wa kike kujitokeza na kuwania uongozi.
''Watoto wetu wa kike watasema nini iwapo tutajiondoa''?
Anasema kuwa lengo lake kuu ni kuimarisha kilimo katika kaunti hiyo.
Kwengineko wanawake wengine watatu wanaongoza katika kinyang'anyiro cha usineta nchini humo.
Susan Kihika na Margaret kamar ni wagombea wanawake wanaoongoza katika matokeo ya usineta katika kaunti ya Uasin Gishu na Isiolo.
Mjini Nakuru, Susan Kihika ambaye anagombea kupitia chama tawala cha Jubilee anaongoza akiwa mbele ya mgombea wa chama cha ODM Samuel Ogada.
Vilevile Margaret kamar wa chama cha Jubilee anaongoza dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Independent .
Wanawake wengine walioshinda viti vya ubunge ni Mishi mboko wa likoni aliyemshinda Masoud Mwahima, Aisha Jumwa aliyeshinda kiti cha eneo bunge la kilifi na Naisuna lesuda aliyeshinda kiti cha eneo bunge la Samburu magharibi.
Aisha Jumwa wa chama cha ODM aliwashinda wanamume saba kushinda kiti cha eneo bunge la Malindi .
Phillip Charo of Jubilee Party got 14,219 votes while Willy Mtengo (Independent) was third with 6,658 votes.
Na katika kaunti ya Homabay Historia imeandikishwa baada ya wanawake watatu kuibuka washindi katika viti vya maeneo bunge ya kaunti hiyo.
Wabunge hao ni Millie Odhiambo wa Suba, Lilian Rongo wa Rangwe na Dr Eve Obara wa Kabondo Kasipul.
Watatu hao waliwashinda wagombea wengine katika mchujo wa chama cha upinzani cha ODM uliotawaliwa na wanaume katika jimbo hilo.