Mwanamume anayeongoza kwa ukweaji mwamba , Adam Ondra, amefanikiwa kukwea ''mwamba mgumu zaidi duniani
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24, alikwea mwamba huo nchini Norway kwa dakika ishirini baada ya kufanya mazoezi kwa miaka miwili

Adam aliambia Newsbeat, ukweaji wa mwamba huo ulimuacha kinywa wazi ,'' kile nilichohisi ni machozi kutoka kwa macho yangu.''
Mwamba huo uliopo katika eneo la Flatanger, nchini Norway huorodheshwa na wakweaji wengi kama mwamba mgumu zaidi na ni eneo hatari kwa wakweaji kama Adam lakini ambao wana ndoto za kukamilisha ukweaji wa mlima huo.
Adam Ondra
Image captionAdam Ondra
Nilijihusisha na ukweaji kwa sababu wazazi wangu walikuwa wakweaji na walienda nami nikiwa mdogo na nilitaka kuukwea milima kama wao,'' Adam aliambia Newsbeat.
''Niko na umri wa miaka 24, nimekuwa nikikwea milima kwa miaka 20. Nimekwea milima hasa nchini Uhispania na Norway, ambapo nimekuwa nikijifunza.
''Kila njia ina kiwango chake katika mchezo wa ukweaji, njia rahisi ni 1 na ile ngumu zaidi ni 9c'', alisema
''Nimekwea njia ngumu zote tatu za kiwango cha 9b+ ulimwenguni lakini nimeangazia sana njia hiyo ya Norway.
ilinichukua wakati mwingi kujifunza kukwea lakini umekuwa wakati mzuri kwangu.''
Adam anayetoka Czech Republic , mara ya kwanza alitembelea mwamba huo mwanzoni mwa mwaka 2016 na kuchimba alama tofauti ambazo zingemzuia kupata majeraha.
Adam OndraHaki miliki ya pichaAFP
Image captionAdam Ondra
Alitumia karibu siku 50 huko Norway, na amekuwa akirudi mara kwa mara kujaribu njia hiyo ngumu kukwea mwamba huo.
''Baada ya mara kadhaa nikaanza kufahamu kile nilichohitaji kufanya,'' alisema
''Mimi ndiye mtu wa kwanza kujaribu kukwea njia hii ngumu na nitaipatia kiwango cha 9c na hakuna yeyote aliyependekeza hilo hapo awali.
'' Ni njia iliyongumu sana kwangu , nilipomaliza kuukwea mwamba huu mgumu, nilijawa na furaha na nikasherehekea.
''Kwa wakati huu nilifika kileleni lakini nilibaki nimening'inia kwenye kamba , na nilihisi machozi kwenye macho yangu, hata sikuweza kupiga kelele.
''Bado nina miradi mingi kukamilisha kote ulimwenguni.''
Miongoni mwa miradi hiyo ya 2020 ya Olimpiki itakayoandaliwa mjini Tokyo, ambapo mchezo wa ukweaji utashirikishwa kwa mara ya kwanza.
Adam amesema si lengo lake kwa sasa , lakini ataanza mafunzo ya mashindano hayo kabla ya michezo hiyo ya Tokyo kuanza.