Kocha wa Klabu ya Atletico Madrid Diego Simeone amezima tetesi za kuhamia klabu ya Inter Milan ya Italia baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu kuendelea kufundisha miamba hiyo ya jiji la Madrid.

Murgentina huyo alikuwa akihusishwa na kuhamia kwa vigogo hao wa Italia, ambao aliwachezea kuanzia mwaka 1997 hadi 1999, lakini ameamua kujifunga na waajiri wake wa sasa.
Simeone anapendwa sana na mashabiki wa Atletico Madrid ambao wamejenga imani kubwa kwake kufuatia kushinda taji la La Liga kama mchezaji na baadaye kocha.
Simeone amesaini mkataba mpya ambao unamfunga Atletico Madrid kwa misimu miwili zaidi, mpaka Juni 30, mwaka 2020 .