Waziri mkuu wa Lesotho{pichani juu} ameelezea mauaji ya mkuu wa kikosi cha jeshi Khoantle Mots'omots'o yaliyofanywa na maafisa wa jeshi kama kitendo cha kurudisha nyuma juhudi za kutafuta amani nchini humo.

Tom Thabane amesema upelelezi unaendelea juu ya tukio hilo lililotokea katika mji mkuu Maseru siku ya Jumanne.
Mashuhuda wanasema, watu wawili waliovalia sare za jeshi waliingia katika ofisi ya Mots'omots'o na kisha kumfyatulia risasi kabla ya wao kuuawa na walinzi wa kiongozi huyo.
Lesotho ipo katika hali ya taharuki, ikiwa na hostoria ya mapinduzi ya kijeshi ya mara kwa mara.