WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harison Mwakiembe amesema kuwepo kwa kituo cha Kamisheni ya Kiswahili cha Afrika Mashariki Zanzibar ni somo ambalo wenzao katika Jumuiya hiyo wamejifunza kwamba amani na utulivu wanayoiona Tanzania imechangiwa sana na uwepo wa lugha moja inayozungumzwa na watanzania wote.
Ameyasema hayo katika uzinduzi wa Kongamano la kwanza la kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki
ilifyofanyika visiwani Zanzibar. Amesema kuwa mwalimu Nyerere aliona mbali alipotangaza kuwa Kiswahili ndio lugha kuu ya kiserikali mara tu alipopata uhuru kwa kutumia mfumo wa elimu wa kumfanya kila mtu aweze kuzungumza Kiswahili.
Amesema kuwa wakati wao ilikuwa mwanafunzi aliemaliza darasa la saba katika Mkoa mmoja hatoweza kufanya mtihani wa Sekondari ndani ya mkoa wake bali atapelekwa katika mkoa mwengine lengo ni kuweza kuifanya lugha hiyo iweze kuenea na amefanikiwa.
“Zamani tulipokuwa tunasoma mwanafuzi akimaliza darasa la saba katika mkoa wa Mbeya hatofanya mtihani wa Sekondari mkoani humo bali atakwenda Mtwara na wa Mtwara ataenda Arusha ilimradi ilikuwa wakati wa likizo ilikuwa kuna mzunguuko mkubwa wa vijana kwenda katika mikoa yao”, amesema mwakiembe.
Hivyo amesema kuwa mchakato huo wa kuwafanya vijana wengi wapoteze lugha zao na kukifanya Kiswahili ndio tumie lugha ya Kiswahili kama ndio lugha yao kuu na hao ndio viongozi wa leo na watu wazima leo na hata wengi wa sehemu ya vijana hao kutokuoa katika mikoa yao.
Aidha ameshauri kuwa Zanzibar iendelee kuwa ni sehemu ya kufanyia makongamano yote ya Kiswahili badala ya kuendelea na utaratibu wa kuznguka kama ilivyo kwa mikutano mengine yanayoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwakiembe amesema kuwa wanajumuiya hao wamekuwa na utamaduni wa kuzunguuka katika mikutano yao lakini kutokana na umuhimu wake ni vyema wakaifanya Zanzibar kuwa ni sehemu maalumu ya kufanyia kongamano hilo kila mwaka. “Tumekuwa na kawaida ya kuzunguka zunguka lakini si kwa Kiswahili mimi nisingependa lizunguke lakini kwa upande wa Kiswahili hebu tuifanye Zanzibar kuwa ni maka kwa lugha hii, amesema.
Hata hivyo amesema kuwa hatua ya kufanyika kwa kongamano hilo na kuzinduliwa kituo cha Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ndani ya Tanzania ni mafanikio makubwa kwa sababu lugha hiyo kila nchi ambayo ni ya Afrika Mashariki hasa Tanzania na Kenya wote wana madai halali kabisa kwamba wamechangia kuwepo kwake. Hivyo amesema kuwa mwanzoni ilikuwa kuna mchakato mkubwa sana na mpaka kufikia Tanzania kufanikiwa na kuweza kushawishi viongozi wakuu wan chi hizo kukubali kuwa Zanzibar ni nchi muafaka ya kuweka hicho kit
0 Comments