Wanachama watatu wa CUF upande wa wanaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba wamefariki dunia katika ajali iliyotokea katika eneo la Zomozi kabla ya kufika Mdaula mkoani Pwani.
Kwa Mujibu wa Msemaji wa chama hicho upande wa Profesa Lipumba, Abdul Kambaya, wanachama watatu hali zao sio nzuri na wamehamishiwa katika hospitali ya Tumbi wakati wengine wanne hali hao zinaendelea vizuri katika Hospitali ya Chalinze.
Kwa Mujibu wa Kambaya, miongoni mwa waliofariki ni Uledi Ramadhani huku wengine wawili juhudi za kuyajua majina yao zinaendelea. Wanachama hao walitoka kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa wabunge saba wa chama hicho mjini Dodoma jana.
0 Comments