Mwanahabari nchini India ambaye pia ni mwanasiasa wa mrengo wa kushoto nchini humo ameuawa kwa kupigwa risasi.
Gauri Lankesh aliyekuwa akihariri gazeti la kila wiki, alikutwa katika bwawa la kuogelea nyumbani kwake mjini Bangalore,huku damu zikiwa zimetapakaa.

Wanafamilia wakiomboleza
Image captionWanafamilia wakiomboleza
Polisi wanasema amepigwa risasi mara mbili kichwani na watu waliovamia nyumbani kwake wakiwa na pikipiki.
Serikali imeyataja mauaji hayo kama kupunguza uhuru wa demokrasia.
Hakuna aliyekamatwa mpaka sasa.